Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bakar Hamad Bakar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: - Je, kwa kiasi gani mifumo ya TEHAMA inasaidia kuongeza uwajibikaji wa Watumishi wa Umma nchini?
Supplementary Question 1
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na vilevile namshukutu na kumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu haya mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na changamoto ya muda mrefu ya kusomana kwa mifumo ambayo Mheshimiwa Waziri ameitaja na mifumo mingine ya Serikali. Kwa kuwa kuna ahadi na mapendekezo mbalimbali ambayo yametolewa ndani ya Bunge na nje ya Bunge ya kwamba mifumo hii inakwenda kuunganishwa, sasa nataka kujua, katika utekelezaji huu Serikali imefikia wapi ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi kazini? Ahsante.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza, nampongeza Mheshimiwa Bakar Hamad kwa kufuatilia habari ya mifumo kusomana. Kwa kweli hili ni agizo la Mheshimiwa Rais katika nyakati mbalimbali kuhakikisha mifumo inasomana. Vilevile, katika kuchukua hatua, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia taasisi yake ya e-GA ikishirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imejenga mfumo wa kuwezesha mifumo kusomana ambao unaitwa Government Enterprises Service Bus. Mfumo huo mpaka kufikia tarehe 30 Septemba, 2024 umesaidia taasisi zaidi ya 175 mifumo yao kusomana na kubadilishana taarifa, ikiwemo ile mifumo muhimu ya Hakijinai, Polisi, Mahakama na PCCB. Nakushukuru.
Name
Dr. Alice Karungi Kaijage
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: - Je, kwa kiasi gani mifumo ya TEHAMA inasaidia kuongeza uwajibikaji wa Watumishi wa Umma nchini?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa vile mifumo hii pia inatumika kupima utendaji kazi wa watumishi, je, Serikali ina mpango gani kwa wale watumishi ambao wako pembezoni ambako hakuna mitandao na pia wale wenye kazi kubwa ili zile asilimia wanazowapimia kufika waweze kupanda vyeo na shughuli nyingine? Ahsante.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Dkt. Alice Kaijage kwa kufuatilia masuala yanayohusu watumishi. Naomba nimhakikishie kwamba, tulipoanza zoezi la kuwapima watumishi, hatukupata malalamiko ya watumishi kushindwa kuingia kwenye mfumo wa PEPMIS kwa maana ya kujipima.
Mhshimiwa Spika, hata hivyo, kwa kutambua kwamba maeneo mbalimbali ya nchi yanakumbana na changamoto ya mitandao, Ofisi ya Rais, Utumishi imeendelea kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, katika programu yao ya Tanzania ya Kidigitali, kuhakikisha minara inajengwa nchi nzima na mawasiliano yanakuwepo ili watumishi wa umma nao watakapokuwa wanatumia mifumo yao katika kujipima, wasiweze kupata changamoto, nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved