Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ameir Abdalla Ameir
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza: - Je, ni tafiti ngapi za mbegu za mazao ya kilimo zimefanyika hivi karibuni na kuleta matokeo chanya ?
Supplementary Question 1
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR: Mheshimiwa Spika, napenda kujua, ni miradi ipi ya kiutafiti wa mbegu bora mpya na zenye kuhimili mabadiliko ya tabianchi kati ya hiyo miradi 52 ambayo Mheshimiwa Waziri ameizungumzia hapo imetekelezwa kwa pamoja kati ya taasisi zetu hizi mbili za kiutafiti wa kilimo baina ya TARI kwa Tanzania Bara na ZARI kwa Tanzania Zanzibar na hatimaye imeleta matokeo chanya? Hayo matokeo chanya ni yapi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tuna miradi 93. Tuliyopata matokeo chanya ni maradi 52, na sehemu ya mradi ni kama nilivyoeleza hapo. Kwa mfano, mbegu za mahindi kuna T104 na T105 ambazo zimeonesha zina matokeo mazuri sana na zinafanya kazi kwenye takribani mikoa 14. Kwa hiyo, hizo ni miongoni mwa mbegu ambazo tumezifanya.
Mheshimiwa Spika, tumekuwa na ushirikiano mzuri kati TARI pamoja na ZARI katika utafiti hususan katika zao la karafuu, utafiti bado unaendelea. Nimthibitishie tu kwamba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo hili limekuwa likifanyika kwa sababu matokeo yote yanayoleta tija yamekuwa yakileta manufaa kwa wakulima wetu.
Name
Stella Ikupa Alex
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza: - Je, ni tafiti ngapi za mbegu za mazao ya kilimo zimefanyika hivi karibuni na kuleta matokeo chanya ?
Supplementary Question 2
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na tafiti zinazoendelea kufanyika na pamoja na mbegu mpya ambazo zinaendelea kugundulika, je, Serikali ina mkakati gani wa kuzilinda mbegu zetu za asili, nikitolea mfano wa mbegu ya mbegu ya ule mpunga wa Kilombero, ama mchele mzuri wa Kyela unaonukia ambayo imetoweka sasa hivi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba moja ya jukumu kubwa ambalo TARI wanalo, wanapofanya tafiti ni wanazifanya kupitia mbegu zetu za asili zikiwemo kulinda uasili wake. Kwa hiyo, katika sehemu kubwa ya tafiti zile ni kuhakikisha kuwa mbegu zile ambazo zilikuwa labda zinaathiriwa sana na magonjwa ama hali ya hewa, zinaongezwa tija, kwamba mbegu ni ile ile ya asili, isipokuwa tunachotaka sisi iongeze tija, hususan mavuno yaliyo bora pamoja na kukabiliana na magonjwa. Kwa hiyo, hilo ni jukumu letu, tunafanya hivyo.
Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kwamba, sasa hivi kule Arusha tumefungua benki ya mbegu za asili ambazo tumekuwa tukizihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved