Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Antipas Zeno Mgungusi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Malinyi
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuondoa miradi chini ya shilingi milioni 100 katika Mfumo wa NeST ili kupunguza ucheleweshaji?
Supplementary Question 1
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wakandarasi wengi wale ambao wana sifa za kuendana na mfumo kwenye miradi midogo hawapatikani vijijini, mara nyingi wanatoka mijini. Muda wao wa kuji-mobilize kufika site kutoa huduma unakuwa mwingi na kazi huwa zinachelewa. Je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha kwamba inawapa upekee local fundi au wakandarasi wadogo kutotumia mfumo au kujengewa uwezo ili waweze kutosheleza vigezo vyao kusudi kazi ziweze kufanyika kwa wakati?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Antipas, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba baadhi ya wakandarasi wale wadogo wadogo bado iko changamoto ya uelewa juu matumizi ya mfumo huu, lakini Serikali itaendelea kutoa elimu kwa local fundi na wale wote wenye mahitaji ya matumizi ya mfumo huu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved