Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. DAIMU I. MPAKATE K.n.y. MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, ni Miradi mingapi ya kimkakati imetekelezwa katika Wilaya ya Tunduru?
Supplementary Question 1
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Mji wa Tunduru unakua kwa kasi kubwa sana kwa ajili ya maendeleo ambayo nimeyazungumza pamoja na uwepo wa soko la madini, lakini kuna changamoto soko la mazao mchanganyiko, tulilokuwa nalo kwa sasa halikidhi haja ya mahitaji ya watu wa Tunduru. Je, Serikali ina mpango gani kuisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kujenga soko la kisasa la mazao mchanganyiko ili kuweza kuwahudumia wananchi wa Tunduru?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Jimbo la Tunduru Kusini linapakana na Msumbiji. Wananchi walio karibu na Msumbiji wanakuja Tanzania kufuata bidhaa mbalimbali za madukani. Je, Serikali haioni haja sasa ya kuweka soko la kimataifa katika Kijiji cha Lukumbule ili kurahisisha biashara kati ya Msumbiji na Tanzania?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge kama anavyofahamu tupo katika kipindi cha kuandaa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka 2025/2026. Kwa hiyo, tunayachukua haya kama mawazo yake kwamba ni muhimu yaingie katika mpango ujao, lakini nakiri kwamba yote haya ambayo ameyaeleza, uwepo wa soko la mazao ni muhimu, na pia uwepo wa soko la kimataifa kama ilivyo katika maeneo mengine kama Namanga, ni muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachukua katika mpango ujao wa maendeleo tuingize, naye kupitia kikao hiki ambacho kinaendelea hapa atoe mchango wake kama ushauri, nasi Serikalini tuchukue ili kutengeneza taratibu zetu na mipango, basi iingie katika mpango wa fedha ujao, nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved