Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watu wasio na ulemavu kujiunga na vyuo vya watu wenye ulemavu?
Supplementary Question 1
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa ruhusa yako naomba nitoe pongezi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha vyuo vyote vya wenye ulemavu ikiwemo kile cha Yombo, Ilala - Dar es Salaam, Masiwani – Tanga na Luwanzari - Mwanza vyuo hivi vilikuwa katika hali mbaya na sasa vina mazingira mazuri sana pongezi kwake Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulijali kundi hili muhimu la watu wenye ulemavu. Sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kwenye vyuo hivi vya wenye ulemavu ambavyo nimevitaja hapo mwanzo vina wanafunzi ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali na kuna wenye ulemavu wa viungo ambao wana changamoto kubwa ya kufanya zile kazi za kiufundi, lakini pia idadi ya walimu kwenye vyuo hivyo hailingani na idadi ya wanafunzi kwa sababu wanafunzi wale wanatakiwa sasa idadi yao iwe mwanafunzi mmoja kwa mwalimu mmoja au wanafunzi wawili kwa mwalimu mmoja.
Je, Serikali haioni haja sasa yakuvifanya hivi vyuo viwe inclusive ili wanafunzi wale waweze kusaidiana wenyewe kwa wenyewe? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa kwenye Shule ya Msingi Wailesi iliyopo katika Wilaya ya Temeke kuna kitengo cha watoto wenye ulemavu wa ubongo ambao wao wanasoma pale kwenye elimu jumuishi na wanapofikia hatua fulani wanapelekwa kwenye kujifunza mafunzo ya ufundi na chuo hicho hakina mapato yoyote wala hakipewi ruzuku yoyote kutoka Serikalini.
Je, Mheshimiwa Waziri muhusika yupo tayari kufuatana na mimi kwenda kwenye hiyo Shule ya Msingi Wailesi iliyopo katika Wilaya ya Temeke? (Makofi)
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM K.n.y. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Mariam kwa kufuatilia watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inawajali sana watu wenye ulemavu na ndiyo maana imejenga shule ambazo mchanganyiko na watu ambao wasio walemavu ili waweze kuwasaidia katika kazi wanazozifanya na kuwapa vifaa vya kuwasaidia ili waweze kuwa na uelewa rahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, Serikali ipo tayari na Wizara husika kwenda kwenye chuo hicho kuangalia mazingira yaliyopo ili kuweza kuwasaidia kwa umakini, ahsante. (Makofi)
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watu wasio na ulemavu kujiunga na vyuo vya watu wenye ulemavu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wetu wa Iringa una idadi kubwa sana ya watu wenye ulemavu katika wilaya zake zote, lakini wamekuwa wakimaliza shule hawajui utaratibu wa kujiunga kwenye vyuo. Je, ni utaratibu gani unatumika ili waweze kwenda kujiunga kwenye vyuo vya ufundi?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM K.n.y. WAZIRi MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa dkt. Ritta, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua suala la watu wenye ulemavu na kama nilivyosema mwanzo Serikali inawajali watu wenye ulemavu kwa kuzingatia katika kupata elimu kuna vifaa mbalimbali ambavyo vinawasaidia na kufika shule kuna mazingira ambayo yanawasaidia kuwahakikishia wanapata elimu hiyo na walemavu wote wanatakiwa wajiandikishe kama sensa iliyopita ilivyoeleza, inawatambua walemavu wapo wangapi na kujua kwamba shule za walemavu tuchukue watu wangapi, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved