Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 1
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kama inavyoonesha kwenye jibu la Serikali hapo kituo hiki hakuna wodi hata moja, je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kujenga angalau wodi moja ya akina mama? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kituo hiki kina changamoto ya wataalamu wa mionzi kama ilivyo Hospitali ya Mji wa Nanyamba ina X-ray lakini hakuna mtaalamu wa mionzi. Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka wataalamu katika wilaya hizi mbili za pembezoni? Nakushukuru. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Kituo hiki cha Afya cha Mkwedu kina upungufu wa miundombinu muhimu ambayo inatakiwa kuwepo ili kukidhi vigezo vya kuwa kituo cha afya zikiwemo wodi za wazazi, lakini na majengo ya upasuaji na majengo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tumechukua hoja hii tutakwenda kuiweka kwenye mipango yetu kuhakikisha kwamba tunatafuta fedha haraka iwezekanavyo ili kwenda kujenga jengo la wazazi, lakini pia jengo la upasuaji ili wananchi wa Kata ya Mkwedu wapate huduma zile ambazo zinafanana na kituo cha afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili kuhusiana na upungufu wa watumishi wa X-ray na Ultrasound, ni kweli tuna changamoto ya watumishi hawa katika soko wapo wachache sana na kila kibali cha ajira kinapojitokeza kipaumbele ambacho Serikali inatoa ni kuanza kuajiri kwanza wataalamu ambao kwenye soko wapo wachache wakiwemo hao wa Ultrasound pamoja na wa X-ray. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba kwenye kibali ambacho Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekitoa hivi karibu tutahakikisha wale ambao wanasifa wanakwenda kwenye Halmashauri hii ya Newala ili kupunguza upungufu wa watumishi wa X-ray na Ultrasound, ahsante. (Makofi)
Name
Aysharose Ndogholi Mattembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 2
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga wodi za watoto wachanga katika vituo vya afya vya mkoa wangu wa Singida ili kunusuru vifo vya akina mama na watoto? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ramani za ujenzi wa vituo vya afya za sasa zinazingatia sana uwepo wa wodi au vyumba kwa ajili ya watoto wachanga. Kwa hiyo vituo vyote vya afya ambavyo vimejengwa zaidi ya 878 mpaka sasa vina wodi na vyumba maalumu kwa ajili ya watoto wachanga. Vituo vya afya ambavyo vilijengwa siku za nyuma vina upungufu wa miundombinu hiyo na tayari vimewekwa kwenye mpango ule wa ukarabati na upanuzi wa vituo vile kongwe tutahakikisha sehemu ya miundombinu ni pamoja na vyumba hivyo vya watoto wachanga, ahsante. (Makofi)
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 3
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Kilolo kuna Vituo vya Afya vya Nyalumbu, Ilula, Ng’uluwe na Ruaha Mbuyuni havina vifaa tiba, nini mkakati wa Serikali kupeleka vifaa tiba katika vituo hivyo vya afya? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka miwili ya fedha 2022/2023 – 2023/2024 Serikali hii ya Awamu ya Sita imeshapeleka fedha kwenye halmashauri zote 184 zaidi ya shilingi bilioni 93 kwa ajili ya vifaa tiba na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imepata fedha mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya vifaa tiba na mwaka huu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya vifaa tiba.
Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kumwelekeza na kumsisitiza Mkurugenzi na Mganga Mkuu wa Halmashauri kuweka kipaumbele kwenye vituo vya afya ambavyo vinaupungufu mkubwa zaidi wa vifaa tiba ili fedha ile inunue vifaa hivyo viende kutoa huduma katika vituo ambavyo vina upungufu mkubwa, ahsante. (Makofi)
Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 4
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Iwondo ili wananchi wa Kata ya Iwondo waanze kupata huduma? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, vipo vituo vya afya ambavyo vimejengwa kwa awamu ya kwanza ambavyo vilipelekewa shilingi milioni 500 au shilingi milioni 400 na miundombinu muhimu ya majengo matano imekamilika, lakini vituo hivyo vyote tutaviingiza kwenye ujenzi wa awamu ya pili ambao utahusisha ujenzi wa wodi, lakini pia wodi ya wanaume, wanawake pamoja na wodi ya watoto.
Kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Malima kwamba tukifika awamu ya pili tutaipa kipaumbele pia kituo hicho cha afya ili tuweze kujenga miundombinu ambayo inapungua, ahsante.
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 5
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Kituo cha Afya Ngome, Kituo cha Afya Ipogolo na Kituo cha Afya Isakalilo ni vile vituo ambavyo vimejengwa zamani, havina wodi za kisasa kwa ajili ya kujifungulia. Je, Serikali mnaweza mkatusaidia tupate wodi hizo kwa sababu pia tunahitaji huduma hiyo kwa haraka?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tumechukua hoja ya vituo vya afya vya Manispaa ya Iringa na Jimbo la Iringa Mjini na kwa bahati nzuri tumeshafanya ziara nafikiri Isakalilo pale tuliona, tulishatoa maelekezo na nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutatafuta fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo, ahsante. (Makofi)
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Mkwedu – Newala?
Supplementary Question 6
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Jangalo, Mpendo na Lahoda ni kata za mpakani, mwaka 2003 Serikali ilifanya tathmini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, nataka kujua ni lini sasa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kata zote za kimkakati tayari tumeshazianisha kwa awamu, tulishaanza na awamu ya kwanza mwaka wa fedha 2021/2022, tupo awamu ya pili mwaka wa fedha 2023/2024. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutatafuta fedha na kwenda kujenga vituo vya afya hivyo kwa awamu kadiri ambavyo tumeweka mpango mkakati katika nchi nzima, ahsante.