Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Alice Karungi Kaijage
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SILYVESTRY F. KOKA aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mamlaka ya Maji Mkoa wa Pwani ili kuondoa changamoto ya maji maeneo mengi ya mkoa huo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Silyvestry Francis Koka, tunashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto zimeendelea kuwepo Mkoa wa Pwani kwenye suala la maji, je, lini Serikali itaanza kujenga Mradi wa Maji uliopo Pangani ukizingatia toka mwaka jana mwishoni tulisaini mkataba? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Serikali ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maji nchini kote. Vilevile kwa upande wa Mradi huu wa Pangani, Serikali tayari ipo katika hatua nzauri kabisa za kuendelea na utekelezaji wa mradi huu. Nimuombe tu Mheshimiwa Mbunge atupatie nafasi Serikali ili tuhakikishe kwamba mradi huu unakamilika na wananchi wa Pwani na maeneo maeneo yote yanayozunguka mradi huo wapate huduma ya maji safi na salama, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved