Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Primary Question
MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, lini Serikali itabadili Kanuni ili Makamu Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya watumikie kwa miaka mitano badala ya mwaka mmoja?
Supplementary Question 1
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Bunge lako hili ni mdau muhimu sana na hoja hii imetokea Bungeni kwako hapa; na kwa kuwa, pia utaratibu huu unaziingiza halmashauri katika gharama kubwa kila mwaka kuandaa Uchaguzi wa Makamu Wenyeviti; na pia, kwa kuzingatia R4 za Mheshimiwa Rais: Je, Serikali, haioni kwamba kuna haja ya kuchukua hoja hii na kuifanyia kazi? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali inaona umuhimu wa kuchukua hoja hii ya Mheshimiwa Mbunge Ndaki na kuifanyia kazi. Ndiyo maana tumesema tutafanya tathmini kujiridhisha na kushirikisha wadau mbalimbali kwa sababu Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti na Naibu Meya kila mwaka unasaidia kuwapa exposure Waheshimiwa Madiwani walio wengi kuwa tayari kuwa Wenyeviti au Makamu Wenyeviti kwa kipindi kingine. Kwa hiyo, tunaichukua hoja hii kwa ajili ya kuifanyia kazi, ahsante sana.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, lini Serikali itabadili Kanuni ili Makamu Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya watumikie kwa miaka mitano badala ya mwaka mmoja?
Supplementary Question 2
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Hili jambo la Makamu Mwenyekiti kuchaguliwa kila mwaka limeleta matatizo makubwa sana kwenye halmashauri. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri anashindwa kufanya kazi kwa kutumia uwezo wake badala yake anakuwa masaa yote ni kujipendekeza kwa Mwenyekiti na Madiwani ili aendelee kuwepo. Kwa hiyo, tunaomba hili jambo lichukuliwe serious, ni jambo baya sana, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri.
SPIKA: Mheshimiwa Mariam Madalu Nyoka, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved