Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, kwanza nasikitika sana kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa sababu, msingi wa swali langu ni kwamba tarafa hii ina kata mbili; Kata ya Negero na Kimbe ambapo wananchi wa kata hizi wanapata huduma Wilaya ya Handeni na Wilaya ya Mvomero na kwa kipindi hiki cha mvua ni kwamba wananchi hawapati huduma hiyo. Swali langu ni kwamba, je, Serikali iko tayari kujenga kituo cha afya cha kimkakati katika Kata ya Kimbe?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, namwomba Mheshimiwa Naibu Waziri atume timu yake ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuangalia adha wanayopata wananchi kwenye huduma hii ya afya katika maeneo hayo, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba tu nimtoe hofu na mashaka Mheshimiwa Omari Kigua kwamba, Serikali inatambua umuhimu wa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Kimbe kwa sababu, wananchi wengi wanahitaji huduma za afya na kituo cha afya kilicho jirani kiko umbali mrefu sana. Kwa hiyo, ndiyo maana tumemwelekeza Mkurugenzi, ameshatenga fedha shilingi milioni 136 na tayari jengo la OPD liko 92%. Kwa hiyo, utaona tayari tumeanza utekelezaji na ni suala tu la kutafuta fedha, tutaendelea kuhakikisha kwamba tunajenga kituo hicho na kinakamilika mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, pili, kuhusiana na kutuma wataalamu, tunafahamu, lakini nitamwelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa pia Mganga Mkuu wa Halmashauri waweze kuleta taarifa rasmi ili tuweze kuongeza kasi ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki cha afya, ahsante.

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 2

MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, naomba kufahamu ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya kwenye Kata ya Mkomba katika Tarafa ya Kamsamba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Juliana Shonza, amefuatilia sana kwa kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo kuhusiana na kituo hiki cha afya. Tumemwahidi na tumekiingiza kwenye orodha ya vituo vya afya vya kimkakati. Kwa hiyo, naomba tu nimhakikishie kwamba tayari Serikali inatambua na inaweka mipango yake kwa ajili ya kwenda kutekeleza ujenzi wa kituo hicho cha afya, ahsante.

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 3

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, nataka kujua, ni lini Serikali itapeleka fedha kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimkakati cha Igamba katika Tarafa ya Igamba, Wilaya ya Mbozi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, natumia nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuanza kutenga fedha za mapato ya ndani, kwa ajili ya kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Kata ya Igamba wakati Serikali pia inatafuta fedha kwa ajili ya kwenda kuwaunga mkono wananchi wa Kata hii, ahsante.

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 4

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, Kata za Mpendo, Jangalo na Lahoda ni kata za mpakani na hakuna kabisa huduma ya vituo vya afya. Naomba kujua, ni lini Serikali itatenga fedha ili kujenga vituo vya afya kwenye kata hizo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nirejee maelekezo ya Serikali na msisitizo wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwamba Wakurugenzi wote katika Mamlaka za Serikali za Mitaa watambue maeneo ya kimkakati na maeneo ambayo wananchi wako mbali zaidi na vituo vya huduma za afya, waanze kutenga fedha za mapato ya ndani ili kuanza ujenzi wa maeneo hayo. Wakati huo walete tathmini na gharama zinazohitajika Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi, kukamilisha vituo hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wa Chemba kwamba waandae na watenge fedha kwenye bajeti, pia waanze ujenzi. Sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tutahakikisha tunakamilisha ujenzi wa kituo hicho, ikiwa eneo hilo linakidhi vigezo vya kuwa na kituo cha afya, ahsante.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kituo cha Afya cha Msae, Mwika pale, toka niingie hapa Bungeni nauliza jamani, lini mtakarabati kituo hicho? Tunaambiwa pesa, pesa. Kwa nini vituo vingine vinajengwa, lakini kile cha kwangu hakijengwi? Mnataka mimi nisijisikie vizuri Bungeni hapa! (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa Kimei, kwenye Jimbo la Vunjo hamna kituo cha afya kipya hata kimoja kilichojengwa!

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika…

SPIKA: Ngoja, anza kuongea baada ya kuwasha kisemeo. Hakuna hata kimoja kilichojengwa! Washa kisemeo.

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, tumejengewa vituo vipya viwili, lakini kituo hiki kikongwe, mimi nilizaliwa kwenye kituo hiki…

SPIKA: Nilitaka tu kujua kama hakuna kituo cha afya chochote kilichojengwa. Kwa hiyo, vimejengwa viwili, unataka ukarabati. Haya, ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Kimei, kwenye Jimbo la Vunjo hamna kituo cha afya kipya hata kimoja kilichojengwa!

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika…

SPIKA: Ngoja, anza kuongea baada ya kuwasha kisemeo. Hakuna hata kimoja kilichojengwa! Washa kisemeo.

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, tumejengewa vituo vipya viwili, lakini kituo hiki kikongwe, mimi nilizaliwa kwenye kituo hiki…

SPIKA: Nilitaka tu kujua kama hakuna kituo cha afya chochote kilichojengwa. Kwa hiyo, vimejengwa viwili, unataka ukarabati. Haya, ahsante sana.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imeendelea kuliona sana Jimbo la Vunjo kwa kupeleka fedha kwa ajili ya huduma za afya, ujenzi wa vituo, zahanati, vifaatiba na magari ya wagonjwa. Tutaendelea kufanya hivyo Mheshimiwa Mbunge. Tunatambua kwamba, kituo hiki cha afya ni chakavu na kwa hakika Serikali imeweka mpango wa kukarabati vituo vya afya chakavu baada ya kukamilisha ukarabati wa hospitali za halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, inawezekana Mheshimiwa Mbunge umeona muda mrefu umesema hatujatekeleza kwa sababu tumeweka vipaumbele. Tukarabati kwanza hospitali kongwe za halmashauri ambazo tayari tumeshakarabati kati ya zile 50, tumeshakarabati 31, bado 19 na tunakamilisha mwaka huu wa fedha. Baada ya hapo, tutakuja kwenye vituo vya afya kikiwemo kituo hiki cha afya cha kwako Mheshimiwa Kimei. (Makofi)

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 6

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, je, ni upi mkakati wa Serikali wa kujenga kituo cha afya katika Tarafa ya Vwawa, Eneo la Ihanda ambacho kitatumika pamoja na Ipunga na Ukwile? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kimkakati ambayo yanakidhi vigezo vya kuwa na vituo cha afya, yanajengewa vituo hivyo vya afya kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, ikiwa vigezo vinatimia, tutahakikisha tunatenga fedha, tunajenga kituo cha afya ili wananchi wapate huduma bora za afya, ahsante.

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Tarafa ya Kimbe?

Supplementary Question 7

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Mtaa wa King’azi na Mtaa wa Saranga, wananchi hawana kabisa huduma ya afya na wanahudumiwa chini ya miti katika Ofisi za Serikali za Mitaa. Pamekuwa na ahadi ya Serikali za miaka miwili kukamilisha maboma katika mitaa hii miwili. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha tukamilishe maboma yale? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge, amefuatilia lakini nilishamshauri pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa sababu ya uwezo wa mapato yao ya ndani, wana uwezo wa kukarabati na kuwezesha zahanati ile ianze kutoa huduma.

Mheshimiwa Spika, fedha za mapato ya ndani ni fedha za Serikali, kwa sababu kumekuwa na kasumba ya baadhi ya watendaji kuamini kwamba fedha ya Serikali ni fedha inayotoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI au Serikali Kuu. Fedha ya mapato ya ndani ni fedha ya Serikali kama ambavyo fedha nyingine zinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii nimwelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwamba tunampa kipindi cha miezi sita waanze ukarabati na ukamilishaji wa majengo hayo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaambatana mimi na yeye kwenda kukagua pale na kazi ile itakuwa imeanza kupitia mapato ya ndani ya Manispaa ya Ubungo.