Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule ya Sekondari ya Nyalanja Meatu ili kurahisisha ulinzi wa mali na wanafunzi wa bweni wapatao 600?
Supplementary Question 1
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kipaumbele chake toka akiwa Makamu wa Rais cha kuongeza mabweni ili kuongeza idadi zaidi ya watoto wa kike kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita. Ni zaidi ya mabweni manne tumepewa matano, sasa basi kutokana na kutoka bweni moja hadi mabweni saba kuna ongezeko la watoto wengi zaidi, katika miundombinu ya msingi. Swali la kwanza; je, Serikali haioni haja ya kujenga sasa maktaba katika shule hiyo maalum ya wasichana?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kutokana na wale watoto waliokuwepo 80 hatuna bwalo katika miundombinu ya msingi. Je, Serikali haioni sasa ipo haja ya kujenga bwalo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyalanja? Nakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba Shule ya Sekondari ya Nyalanja katika Halmashauri ya Meatu ni moja ya shule ambazo Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, ujenzi wa mabweni na mabweni matano yamejengwa na yanatumika na wanafunzi. Kwa hivyo, idadi ya wanafunzi imeongezeka na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwenye mpango wa SEQUIP awamu hii tumeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga bwalo pamoja na maktaba katika Shule ya Sekondari ya Njalanja. Ahsante.
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule ya Sekondari ya Nyalanja Meatu ili kurahisisha ulinzi wa mali na wanafunzi wa bweni wapatao 600?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari ya Bukongo Jimboni Ukerewe inachukua watoto wa kike kwa kidato cha tano na sita, lakini haina uzio, jambo ambalo limekuwa na athari kubwa sana kwa namna mbalimbali kwa watoto hawa. Je, ni lini Serikali itatenga fedha na kujenga uzio kwenye shule hii ya Sekondari ya Bukongo? Nashukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweka vipaumbele katika ujenzi wa miundombinu ya elimu, tumeanza na ujenzi wa madarasa ili tuweze kuwa na uhakika watoto wetu wote wenye sifa za kwenda shule waingie madarasani. Kazi hiyo imefanyika kwa ufanisi mkubwa tumejenga mabweni na hivi sasa tunakwenda kujenga uzio katika shule zile ambazo zina mazingira hatarishi zaidi kwa wanafunzi. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakapoanza mpango wa ujenzi wa uzio katika shule hizo, tutatoa kipaumbele shule hii katika Halmashauri ya Ukerewe. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved