Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stanslaus Shing'oma Mabula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyamagana
Primary Question
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, Serikali haioni kuwa umefika wakati wa kubadilisha sheria ya mwendo wa magari kutoka kilometa 80 hadi kufikia kilometa 100 kwa saa?
Supplementary Question 1
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini Mheshimiwa Waziri atakubaliana nami kwamba, pamoja na majibu ya Serikali kwa swali langu, lakini miundombinu yetu ya barabara imeimarika sana, hususan barabara kuu. Hizi sheria zilizotunga speed limit ya 50 na 80 kiukweli ni kama zimepitwa na wakati. Sasa hivi tuna magari yanakimbia mpaka speed 280 na yeye kama Naibu Waziri atakuwa shahidi; je, hawaoni sasa uko umuhimu wa lazima wa kubadilisha sheria ya speed 50 kwenda angalau 80 na ile ya 80 kwenda angalau mpaka 100 hadi 120. Ahsante. (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stanslaus Mabula, Mbunge wa Nyamagana kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwango vilivyopo sasa hivi vya kilometa 50 kwa saa na 80 kwa saa viliwekwa baada ya kufanya tathmini ya hali ya barabara na kupokea maoni ya wadau mbalimbali na hatimaye zikawekwa kisheria. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafanya tathmini ya hali ya barabara ilivyo nchini na kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kabla ya kubadilisha sheria hii ya viwango vya 50 kwenda 80 na 80 kwenda 100. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved