Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT.CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango mkakati gani juu ya Kiwanda cha Nyama kilichopo Shinyanga ambacho hakifanyi kazi iliyokusudiwa?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba Serikali ilitumia fedha nyingi sana katika kuwekeza kiwanda hiki. Kwa majibu ya Naibu Waziri anasema kwamba wanaendelea kutafuta mwekezaji mahiri. Swali la kwanza, je, ni lini sasa huyo mwekezaji mahiri atapatikana ili kiwanda kiweze kufanya kazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa toka mwaka 1974 kilivyojengwa hakijawahi kufanya kazi na eneo lipo na majengo yapo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kubadilisha walau matumizi ya hicho kiwanda ili uwekezaji mwingine ukafanyika?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibu la msingi ni kweli kwamba Serikali ilitumia pesa nyingi sana kujenga kiwanda hiki mwaka 1975. Ukweli ni kwamba sasa majengo hayo yamekaa kwa muda mrefu na eneo hilo limekaa kwa muda mrefu bila matumizi. Kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba Serikali inaendelea kutafuta mbia ambaye ana uwezo wa kukifufua kiwanda hiko ili kiweze kufanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu lengo la Serikali ilikuwa ni kusogeza huduma hizo za kiwanda hicho katika eneo hilo la Shinyanga na maeneo ya Kanda ya Ziwa. Kwa hivyo, tuko katika harakati za kuendelea kutafuta wawekezaji. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge kama anaweza akatusaidia pia na sisi tuko tayari kushirikiana naye kuhakikisha kwamba tunapata mwekezaji katika eneo hili atakayefufua kiwanda hiki ili aweze kusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la pili la kubadilisha matumizi, Wizara tutakwenda kuangalia kama tulivyosema kwamba tuko katika hatua za kutafuta mwekezaji, lakini kwa mawazo hayo ya Mheshimiwa Mbunge pia tuko tayari kufuatilia kuona kama tunaweza kubadilisha matumizi. Tutaangalia wapi kwenye tija, kuendelea kutafuta mwekezaji ama kwenda kuangalia namna gani bora zaidi ya kwenda kuboresha katika eneo hilo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved