Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani juu ya eneo lililochukuliwa bila fidia na halijaendelezwa katika Kijiji cha Kasesya mpakani mwa Tanzania na Zambia?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Swali la kwanza; kwa sababu, upo uwezekano mkubwa Serikali imetwaa maeneo mengi ndani ya nchi hii ambayo haijafanyia maendeleo. Je, nini kauli ya Serikali kuhusu maeneo yote ambayo wametwaa na wameshindwa kufanya maendelezo yoyote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa hivi sasa ujenzi unaendelea wa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Matai kwenda Kasesya ambapo kwa hakika eneo lile linaonekana kuwa ni potential kwa sababu liko mpakani. Je, nini mtazamo wa Serikali kuhakikisha kwamba wanalipa fidia na eneo hilo liweze kutumiwa na TRA kwa maana ya kujenga ofisi na nyumba za watumishi? Ili tuondokane na tatizo ambalo lipo la msongamano katika mpaka wetu wa Tunduma.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kauli kwenye maeneo yoyote ambayo hayajafanyiwa maendelezo kama nilivyojibu kwenye swali la msingi ni kwamba kwenye eneo hili ambalo ni specific la Kasesya tumeanza mazungumzo na mamlaka husika ili eneo hili liweze kurejeshwa, kwa wao kushindwa kulifanyia kazi kama walivyolilenga mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, Wizara ya Fedha ione umuhimu wa namna ambavyo inaweza ikapatumia pale kwa ajili ya ujenzi wa jengo la TRA, nadhani Mheshimiwa Waziri amelisikia hili, kwa vyovyote litachukuliwa kwa namna ambavyo Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Mbunge mtaona inafaa kushauriana kwa matumizi ya eneo hili. Ahsante.