Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KUNTI Y. MAJALA K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: - Je, ni lini matengenezo ya pantoni ya MV. Magogoni iliyopo nje ya Nchi yatakamilika na kurejeshwa nchini ili ianze kutoa huduma kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, kivuko hiki kimetumia muda mrefu sana na wananchi wa Kigamboni na watumiaji wengine wa kivuko hiki wameendelea kupata adha kubwa lakini Serikali imekuwa na ahadi zisizotekelezeka. Mheshimiwa Waziri umesema mwaka 2024 kivuko hiki kinakwenda kukamilika. Ni tarehe ngapi? Kwa sababu suala la miaka imekuwa kila leo mnatupa. Tunataka tarehe ili wananchi hawa waondokane na adha hii, ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza ninamkumbusha tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Kigamboni na Dar es Salaam kwa ujumla wake kwamba, ukarabati unaofanyika kwenye MV Magogoni ni kama kukijenga upya, kutokana na ukweli kwamba kivuko kilikuwa kimechoka na tunakileta katika hali ambayo ni mpya kabisa. Ndiyo maana kimeendelea kuchukua muda mrefu ili kuboresha kiwe kivuko cha kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu tarehe ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge; sisi kivuko unaweza ukasema tarehe mbili lakini katika safari ikachukua muda. Tunachotaka kukuhakikishia ni kwamba, kabla ya mwisho wa mwezi Desemba 2024, kivuko kitakuwa kimefika na kuanza kutoa huduma Kigamboni na Dar es Salaam, ahsante. (Makofi)