Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aziza Sleyum Ally
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:- Je, Vibali vya Ujenzi hutolewa baada ya muda gani tangu mwombaji aombe kupewa kibali?
Supplementary Question 1
MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa kuna utaratibu mpya wa kielektroniki wa kupata hivi vibali; je, kibali hicho, kitadumu kwa muda gani tangu kimetolewa? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, wameshatoa elimu katika maeneo mbalimbali kwa wananchi ili waweze kujua kama kuna mfumo mpya; wale wananchi wa Mbeya Mjini waweze kufahamu, wananchi wa Tabora na maeneo mengine waweze kufahamu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mfumo wa Utoaji wa Vibali vya Ujenzi siku za nyuma tulikuwa tunatumia mfumo wa kawaida ambapo mwombaji aliwasilisha makabrasha, ramani na viambatisho muhimu kwa ajili ya kupata vibali.
Mheshimiwa Spika, vibali hivyo vinachukua kati ya siku saba hadi 14 kwa majengo ya kawaida na kati ya siku 14 hadi ya 30 kwa majengo ya ghorofa. Hata hivyo, baada ya kuona kuna maeneo vibali hivi vinacheleweshwa, Serikali ikaanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa TAUSI ambao mwombaji ana uwezo wa kupata kibali ndani ya siku moja, lakini kibali hicho kitadumu muda wote wa ujenzi wa jengo husika.
Mheshimiwa Spika, pili, kuhusiana na elimu, tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi, kwanza kutambua kwamba kuna mfumo huu na namna ya kuutumia. Lakini pia wataalam wote katika halmashauri zetu wamepewa maelekezo ya kuendelea kutoa elimu na kuwasaidia wananchi ili waanze kuutumia mfumo huu muhimu. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved