Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza nafasi za ajira na mafunzo jeshini kwa vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne?
Supplementary Question 1
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kumekuwa hakuna uwiano kati ya wanaoingia kwenye mafunzo na wale wanapata ajira kwenye vyombo vya ulinzi. Je, upi mkakati wa muda mfupi na wa muda mrefu wa Serikali kwa vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT katika kuajiriwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, wanapokuwa kwenye mafunzo pia kumekuwa na changamoto ya miundombinu; je, upi mkakati wa Serikali kukabiliana na tatizo la miundombinu kwa hawa vijana wetu wanaoingia kwenye mafunzo ya JKT? Ahsante.
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la uwiano kama nilivyojibu kwenye swali la msingi inategemea sana nafasi za ajira zinazotolewa na Serikali. Hivyo, haiwezekani watoto waliojiunga na JKT 1,000 wakalingana na ajira ambayo inaweza ikatolewa kwa sababu tu uwezo wa Serikali ndiyo unaweza uka-determine tuchukue watu wangapi kwenda kwenye ajira za kudumu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini miundombinu katika Vyombo hivi vya Ulinzi na Usalama, Serikali imekuwa ikiviangalia kwa jicho la pekee kabisa. Kwa hiyo, hakuna uhakika mkubwa sana juu ya ukosefu wa vitendeakazi na miundombinu ya kimafunzo kwenye maeneo ya makambi ya Jeshi. Namhakikishia tu kwamba Serikali imeweka miundombinu wezeshi kwa vijana wetu ili waweze kupata mafunzo kamilifu yanayoweza kwenda kuwasaidia wanapomaliza mafunzo yao, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved