Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Mfereji wa Shegho ambao unaathiri Wakazi wa Kata ya Kiburugwa Jimbo la Mbagala?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nifanye marekebisho kidogo katika majibu niliyotumiwa hapa. Mfereji huo upo katika Kata ya Charambe, Kilungule, pamoja na Kata ya Kiburugwa tofauti na ilivyoandikwa hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza. Kwa kuwa, mfereji huo umeelekeza maji katika makazi ya wananchi na kusababisha familia zaidi ya 50 kupoteza makazi yao, je, Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia familia hizo kupata makazi ambayo yameelekezewa maji na mfereji huo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri upo tayari kuongozana nami kwenda kujionea familia hizo zinavyoathirika na zinavyoishi katika maisha magumu baada ya kuondokewa na nyumba zao na kuona Serikali itafanya nini, ili kuwarudishia makazi yao?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge, anafanya kazi kubwa sana kuwatetea wananchi wake. Kuhusiana na swali lake la kwanza, naomba nitumie nafasi hii kuikumbusha Halmashauri ya Temeke jukumu lake la msingi la kufanya tathmini ya athari za mvua ambazo zimesababisha mafuriko kwenye mfereji huo na kuathiri wananchi ili kuchukua hatua za kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana swali lake la pili. Mheshimiwa Mbunge, mimi nipo tayari, tutakaa, tutazungumza, tutakubaliana ili niweze kuja kujionea mwenyewe athari ambayo imepatikana kwa wananchi wetu.

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Mfereji wa Shegho ambao unaathiri Wakazi wa Kata ya Kiburugwa Jimbo la Mbagala?

Supplementary Question 2

MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Je, ni lini mifereji ya maji Kata za Kilakala, Makangarawe, Vituka na Buza itakuja kurekebishwa ili athari hizi ambazo zinaendelea ziweze kukoma?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali kupitia miradi yake tofauti tofauti, kwa mfano, Mradi wa DMDP II ambao unakaribia kuanza katika mwaka wa fedha 2024/2025, ina mpango wa kuja kufanya marekebisho na maboresho ya miundombinu katika jimbo lake.


Kwa hiyo, ukiacha tu kwamba kuna fedha za TARURA, lakini bado kuna miradi mbalimbali ya Serikali ambayo inakusudia kuboresha miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Name

Mussa Azzan Zungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Mfereji wa Shegho ambao unaathiri Wakazi wa Kata ya Kiburugwa Jimbo la Mbagala?

Supplementary Question 3

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Dar es Salaam unachangia pato la Serikali kwa zaidi ya 75% na miundombinu yake ya barabara na mifereji imeharibika sana. Kutokana na shida hii mapato ya nchi yanaweza yakapungua kutokana na miundombinu hii kuchelewesha kuendesha uchumi kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini Serikali isitoe Kauli kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri ya Dar es Salaam kuzingatia Sheria ya Manunuzi kwa kutumia Kipengele cha Emergency Procurement, ili barabara hizi zitengenezwe kwa fedha za Serikali ambazo zimechangiwa kutoka kwenye Halmashauri zetu na own source ambazo tunazo wenyewe?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nikizungumzia Manispaa ya Ilala tumeshatenga fedha, lakini mchakato wa kutafuta wakandarasi unachukua muda mrefu sana na kuchelewesha maendeleo ya Dar es Salaam na kuchangia mikoa mingine mapato yanayotoka Dar es Salaam? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa barabara zetu hizi za Wilaya katika uchumi wa Taifa letu. Ni dhahiri kwamba kumekuwa na mvua kubwa sana ambayo imeleta madhara mbalimbali katika miundombinu. Serikali pamoja na kwamba, kuna fedha nyingi ambazo zimetengwa na zinaendelea kutengwa, inakusudia kuhakikisha inaboresha miundombinu hii. Aidha, kutokana na mvua ambayo bado inaendelea kunyesha katika kipindi hiki, hatua za manunuzi zinaendelea huku tukisubiri mvua ikatike ili wakandarasi waingie uwandani kuanza kufanya marekebisho ya barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upekee kabisa kwa sababu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa tayari imeshatoa maelekezo kwa baadhi ya Halmashauri, na hasa za majiji, ziweze kutenga fedha kutoka kwenye own source kwa ajili ya marekebisho mbalimbali ya barabara na kwa sababu, kuna mazingira mengine ambayo barabara zinakuwa hazina mawasiliano kabisa, kwa hiyo, kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa huko awali na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, basi natumia nafasi hii kukumbusha maagizo yale kwamba Halmashauri za majiji ziweze kuchukua hatua za kidharura kwa sababu, tayari zimeshatenga fedha kwenye own source ili ziweze kwenda kufanya marekebisho na hasa kwenye maeneo ambayo mawasiliano yamekatika kabisa na barabara hazipitiki.