Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha mbegu ya Ng’ombe ya asili ya Ufipa haipotei?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila inapofikia msimu wa masika kumekuwa kukitokea milipuko ya magonjwa aina tatu ambayo imekuwa ikiua mifugo hii kwa wingi sana. Aina ya kwanza ya ugonjwa ni black quarter ambayo wafugaji huita ugonjwa wa kamkono kwa sababu ng’ombe huvimba mkono mmoja wa mbele; aidha kulia ama kushoto. Pia, kuna homa ya mapafu na ugonjwa wa ndiganakali ili kuhakikisha kwamba magonjwa haya yanatibika ni pale ambapo chanjo inafanywa kwa wakati.
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba chanjo inafika kwa wakati na inaenezwa katika Wilaya yote ya Kalambo? (Makofi)
Swali la pili, kwa kuwa chanjo hizi zimekuwa na bei kubwa, Je, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba inaweka ruzuku ya kutosha ili wananchi wawe na waweze kumudu kununua chanjo hizi?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anavyosema Mheshimiwa Mbunge. Kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Kandege kwa jinsi ambavyo amekuwa ni mdau mkubwa sana wa hii sekta ya mifugo na katika swali lake hili anataka kujua jinsi ambavyo Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba inadhibiti hii milipuko ya magonjwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya mikakati ya Serikali ni pamoja na kuleta chanjo ya lazima kwa mifugo kuanza mwaka huu na chanjo hii itatolewa bure kwa wafugaji wote walioko ndani ya nchi yetu. Mheshimiwa Rais kupitia bajeti yetu hii ya mwaka 2024/2025 tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 27 ambazo zitaelekezwa kwenye chanjo ya mifugo ambayo itasaidia kuzuia hii milipuko ya magonjwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, solution ya magonjwa haya ya milipuko ni kuhakikisha kwamba wafugaji wetu wanachanja mifugo yao popote pale walipo na chanjo hii itakuwa ni ya lazima, lakini mfugaji atakuwa hachangii chochote, Serikali itasimamia kila kitu katika chanjo hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anataka kujua kwa nini chanjo ziko bei ya juu? Kama nilivyosema, ni kwamba bei ya chanjo inategemea na aina ya ugonjwa ambao mfugaji anataka kuchanja lakini kama nilivyosema kwamba kwa kuanza mwaka huu tutachanja mifugo yetu bure na tunapoendelea wafugaji watapaswa kuwa wanachangia kidogo kigogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii concern yake ya chanjo yetu kuwa juu, basi tutaendelea kuangalia namna ambavyo tutazungumza na wadau wanaoingiza dawa hizi za chanjo ili kuona namna ambavyo wanaweza wakapunguza bei ya chanjo kwa ajili ya kumrahisishia mfugaji ili aweze kuchanja kwa bei rahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, ni kwamba wafugaji lazima wafahamu kwamba chanjo hizi ni lazima ili kuifanya mifugo yetu iweze kuendana na soko la dunia kadri ambavyo maelekezo ya Serikali yamekuwa yakitolewa, ahsante. (Makofi)
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha mbegu ya Ng’ombe ya asili ya Ufipa haipotei?
Supplementary Question 2
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo breed nane tofauti zitakazohifadhiwa, je, zitatosha kwa ajili ya matumizi ya nchi nzima? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi breed nane zinatosha kwa sababu ni mbegu ambazo zimehifadhiwa katika kituo chetu cha NAIC. Mbegu hizi ikifika muda wa matumizi hutumika, siyo mbegu ya breed nane, hii ni aina nane ya mbegu zilizohifadhiwa, lakini mbegu hizo zinazo uwezo wa kuzalisha ng’ombe hata 10,000, kwa sababu ni mbegu ambazo zimehifadhiwa na huzalishwa kwa njia ya uhimilishaji kwa ajili ya kupandikiza mifugo ambayo ipo katika Taifa letu kadri ya mahitaji yanavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, siyo kwamba ni mbegu nane tu, hapana. Hizo ni aina nane za ng’ombe lakini mbegu hizo zina uwezo wa kuzalisha zaidi ya ng’ombe hata 100,000 kadri ambavyo mfugaji anataka.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved