Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza kulipa madeni ya muda mrefu ya watumishi?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanza kulipa madeni. Swali la kwanza; nataka kujua wamejipanga vipi kuhakikisha kwamba wanamaliza madeni yote na mpaka lini watakuwa wameweza kumaliza madeni hayo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; walimu wanalipwa madeni yao kupitia halmashauri. Je, Wizara ya Fedha imejipanga vipi kuhakikisha kwamba inapeleka fedha Hazina ili ziweze kufika kwenye halmashauri zetu kwa wakati? (Makofi)

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, juu ya Serikali imejipanga lini kumaliza madeni? Nataka nilihakikishie Bunge lako kwamba Serikali kwa mujibu wa taarifa na taratibu ambazo tumejipangia tunataka tuhakikishe kwamba madeni ya hawa walimu ikiwezekana hata leo yaishe yote. Sisi kwetu kinachotukwamisha ni wale waajiri ambao hawaleti taarifa kwa wakati na ndiyo maana najibu swali la msingi nilisisitiza kwamba Serikali inatoa wito kwa waajiri wote nchini, kuhakiki na kuwasilisha taarifa za madeni ya watumishi wa umma ili Serikali iweze kuwalipa.

Mheshimiwa Spika, nataka kukushukuru wewe na Bunge lako kwa sababu kila tunapoleta maombi ya bajeti kwa ajili ya malipo ya malimbikizo ya madeni yanayotokana na kazi za kiutumishi mmekuwa mnatupitishia na hivyo kutuwezesha kuweza kulipa.

Mheshimiwa Spika, narudia tena Wabunge wenzangu tuendelee kuwambusha waajiri hasa wakurugenzi katika halmashauri zetu kuendelea kuwasilisha taarifa zinazohusu madeni ya watumishi ili kutatua kilio hiki cha watumishi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili juu ya Wizara ya Fedha imejipangaje. Wizara ya Fedha imekuwa inaleta fedha kwa wakati na kila tunaposema kwamba tunahitaji kulipa imekuwa inafanya hivyo na ndiyo kupitia mfumo huu wa HCMIS fedha zinakuja na madeni katika zile taarifa yanalipwa, ahsante sana.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza kulipa madeni ya muda mrefu ya watumishi?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali ya nyongeza. Kada ya Manesi ni kada ambayo inadai madeni mengi sana hasa fedha za ziada kwa kufanya kazi za ziada. Je, ni lini Serikali itahakikisha manesi hawa wanapata fedha kwa wakati? (Makofi)

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mwakagenda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sisi ndani ya Ofisi ya Rais, Utumishi tunafanyakazi kwa taarifa, naendelea kusisitiza tena kama nilivyoeleza katika jibu la msingi, madeni yote yanayodaiwa na watumishi wa umma naomba yawasilishwe katika ofisi yetu mapema iwezekanavyo ili tuweze kuyalipa.

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza kulipa madeni ya muda mrefu ya watumishi?

Supplementary Question 3

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itawalipa madeni yao wakufunzi wa vyuo vya ualimu, madeni hayo yameshahakikiwa na yanajulikana lakini bado hawajalipwa. Nakushukuru.

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kama itapendeza Bunge lako naona taarifa za kundi fulani wanadaiwa, mara kundi fulani linadai, mara kundi fulani linadai zimekuwa ni nyingi sana.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Waheshimiwa Wabunge pamoja na kazi yetu ya Kibunge ni wakubwa katika maeneo yetu ni viongozi katika maeneo yetu, hebu tutumie nafasi hizi kuleta taarifa hizi pia ndani ya ofisi zetu. Tunayo nafasi kama viongozi ndani ya umma kuzileta taarifa na ofisi yetu mkaidai matokeo ya taarifa hizo, lakini narudia tena kupitia mfumo wa HCMIS tumeendelea kukusanya taarifa za madeni zinazodaiwa ndani ya Serikali na tumeendelea kulipa kutokana na uwepo wa fedha zinazotengwa na bajeti ambayo inapitishwa na Bunge lako.

Mheshimiwa Spika, nataka nilihakikishie Bunge lako, Serikali inayoongozwa na Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais wetu ipo kwa ajili ya kuhakikisha haki ya watumishi wa umma inapatikana kwa kulipa madeni yao ndani ya muda. Niendelee kusisitiza tena na kutoa wito kwa waajiri, leteni taarifa.