Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martha Nehemia Gwau

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA N. GWAU aliuliza: - Je, kuna Kampuni ngapi nchini za kutoa taarifa za mikopo (credit reporting company) zinazoangalia hali ya kifedha ya mkopaji na uwezo wake wa kulipa?

Supplementary Question 1

MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa taarifa za wakopaji ni muhimu kwa financial institutions zote. Je, na hizi microfinance ndogo ndogo nazo zinapeleka taarifa za wakopaji BOT?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ili kuepuka default rate kwa financial institution zetu. Je, BOT wana-update hizo taarifa kwenye credit reference kwa muda gani; kwa wiki au kwa mwezi kwa sababu tunajua wakopaji wanakopa kila siku, nashukuru. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Martha, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, taasisi zote za fedha kubwa na ndogo zinatakiwa zipeleke taarifa sahihi kwenye kanzidata inayosimamiwa na BOT.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kila baada ya mwezi taarifa hizo zinapokelewa na kusambazwa kwa taasisi zinazohusika. Ahsante.