Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza:- Je, Serikali inawasaidia vipi wakulima ambao mazao yao yameharibiwa na mafuriko?

Supplementary Question 1

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; katika mafuriko haya yaliyotokea hasa Bonde la Ziwa Rukwa kuna skimu za umwagiliaji kama Skimu ya Tumaini Ng’ongo, Skimu ya Melepa, Skimu ya Sakalilo na Ilemba ziliharibiwa na ndiyo tegemeo kubwa kwa wananchi wa maeneo haya ya Bonde la Ziwa Rukwa. Nataka kupata commitment ya Serikali wana mpango gani wa kwenda kutengeneza skimu hizi za umwagiliaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Bonde la Mto Ilembo katika Kata ya Mpui ni bonde ambalo linategemewa sana na wakulima wa kata hiyo na wameathirika sana na mafuriko hayo na tayari wameshaenda kufanya upembuzi yakinifu. Ni lini Serikali italeta fedha kujenga Skimu katika bonde hilo la Mto Ilembo? Nakushukuru. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba sisi kama Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tunafanya tathmini katika maeneo yote ambayo yameathirika zikiwemo Skimu za Milepa ambapo Mheshimiwa Mbunge anatokea na nimthibitishie tu kwamba tutarekebisha maeneo yote ambayo yameathirika ikiwemo katika jimbo lako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu fedha katika Bonde la Mto Ilemba ambako tunafanya tathmini, tukishamaliza tathmini tutangaza tender na baada ya hii kazi maana yake kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha ujao kazi itakuwa imeanza katika eneo lako. Kwa hiyo nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi wake kwamba tutaifanya kazi hiyo. Ahsante. (Makofi)