Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Daraja la Kijiji cha Lihale na Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kuunganisha Mbinga Vijijini na Peramiho?

Supplementary Question 1

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri yenye kutia moyo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, daraja hili kila mwaka limekuwa linapoteza watu na hivi karibuni watu watatu wamekufa maji watatu. Je, Serikali kupitia Jeshi la Wananchi haiwezi kutuletea daraja la dharura ili liweze kupitika wakati huu tukisubiri mipango mizuri ya Serikali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali ilitenga fedha shilingi bilioni mbili, kwa ajili ya kujenga daraja la kuunganisha Kingoli, Kata ya Litumbandyosi pamoja na Kijiji cha Machimabharafu, Ibumi, Wilaya ya Ludewa, kwa muda mrefu ujenzi wa daraja hili unasuasua. Je, lini sasa daraja hili litakamilika ili kuleta furaha kwa wananchi hawa, wafa maji karibu kila mwaka?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, napokea masikitiko yake kuhusu changamoto wanazopitia wananchi wake katika Jimbo hili la Mbinga Vijijini. Ninaomba nimpe faraja Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali tayari imeshatenga bajeti ya shilingi bilioni 2.9, kwa ajili ya kujenga Daraja katika Mto Ruhuhu. Mpaka muda huu tayari shilingi bilioni 1.9 zimeshatengwa na tayari awamu ya kwanza ya ujenzi inatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nichukue nafasi hii kumkumbusha Meneja wa TARURA wa Mkoa na wa Wilaya, waweze kusimamia utekelezaji wa mradi huu ili uweze kwisha kwa wakati na wananchi waweze kutumia Daraja hili la Mto Ruhuhu waepukane na changamoto na adha wanazozipata kutokana na mazingira yaliyopo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, Timu ya Wilaya na ya Mkoa ya TARURA imepokea maelekezo haya kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa mradi huu kwa haraka.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Daraja la Kijiji cha Lihale na Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kuunganisha Mbinga Vijijini na Peramiho?

Supplementary Question 2


MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali italeta fedha, kwa ajili ya ujenzi wa madaraja zaidi ya 10 yaliyoathiriwa na Mvua za El-Nino katika Barabara ya Ntikimwaga – Tandawale?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutoa fedha kwa utaratibu wa fedha za dharura. Mpaka sasa hivi Serikali imetumia jumla ya shilingi bilioni 84, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ambayo imeharibiwa na mvua za El-Nino. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali inaendelea kufanya mapitio na tathmini, ili iweze kufikia maeneo mengi zaidi ambayo yameathirika na mvua za El-Nino. Mheshimiwa Mbunge, nimhakikishie Serikali itafika katika madaraja aliyoyataja ili iweze kuyafanyia ukarabati na wananchi waweze kupata miundombinu bora.

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Daraja la Kijiji cha Lihale na Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kuunganisha Mbinga Vijijini na Peramiho?

Supplementary Question 3

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya kutoka Kiponzero kwenda Wasa ina mashimo makubwa sana. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za dharura ili tutengeneze makalavati na kufukia hayo mashimo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Kiswaga kwamba, Serikali itaendelea kufikia maeneo mbalimbali ambayo yameathirika, pamoja na barabara ambazo zimeathirika kwa kiwango kikubwa, ili kuweza kuzirekebisha na kuweza kupitika. Kila mwaka wa bajeti, Serikali inatenga shilingi bilioni 21, kwa ajili ya fedha za dharura, ili kufikia maeneo kama haya. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali itakuja kufika katika Jimbo lako kwenye maeneo uliyoyataja, kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara hizi.

Name

Kasalali Emmanuel Mageni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Daraja la Kijiji cha Lihale na Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kuunganisha Mbinga Vijijini na Peramiho?

Supplementary Question 4

MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali italijenga upya na kwa ubora zaidi, Daraja la Mto Maloha ambalo hivi karibuni lilisombwa na mafuriko na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika Kata za Bugando na Mwabanza?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua mazingira ambayo yanajitokeza, ambapo madaraja yanasombwa na maji, miundombinu inaharibika na mawasiliano yanakatika. Serikali inachukua hatua za dharura na mpaka sasa Serikali imeshatumia jumla ya shilingi bilioni 84 kwa ajili ya kuhakikisha inarudisha mawasiliano maeneo ambayo yameathirika, madaraja yamekatika na hamna mawasiliano. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge dhamira hiyo ya Serikali itaendelea na itakuja kufika katika Jimbo lako kwa ajili ya kuhakikisha miundombinu ya daraja alilolitaja inarejeshwa.