Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza Matibabu ya Wagonjwa Wenye Seli Mundu kwa kutumia Crispr Gene Editing Technology?

Supplementary Question 1

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Gene Editing by CRISPR Cas Technology ni matibabu ambayo yanahusu ku-edit gene ya mtu; kwa maana kwamba mtu anaingia kutibiwa halafu wanai-edit gene ya mtu kuingia kwenye DNA.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Je, pamoja na kwamba wameanza matayarisho Waziri anatuhakikishiaje kwamba mtu haingii kwenye matibabu halafu akafanyiwa editing, vitu vingine ambavyo ni utu wa mtu matokeo yake, procedure ikatoka na mtu wa pili badala ya mtu aliyeingia?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali inajiandaaje kuhusiana na kuleta Muswada Bungeni ili kuwe na sheria maalum zinazoongoza watu wanaoingia kwenye kufanyiwa gene editing ili kuzuia mtu asifanyiwe editing rangi ya macho, rangi ya ywele, rangi ya ngozi na IQ ya mtu na utu wa mtu?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Baba Askofu Gwajima kwa sababu wakati wote yanapotokea mambo mapya na magumu duniani na ya tiba amekuwa akiwa anapaza sauti kutufikirisha zaidi. Nimhakikishie hata kipindi cha Corona alitoa mawazo mazuri sana yaliyotufikirisha, lakini niwaambie kwamba tunaye Jemedari Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaipenda Tanzania na ndiyo maana unaona hata wakati wa Corona alikuja akakubali chanjo wakati muafaka na sasa Watanzania wako salama baada ya hiyo chanjo kufanyika.

Mheshimiwa Spika, juzi mmeona dunia imekuja Tanzania na amepewa nishani ya namna ambayo ni ya kwanza kwa Rais wa Afrika kupewa. Alipewa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na haijatokea kwa bahati mbaya, imetokea kwa sababu ya uwezo wake wa kutafakari masuala ya afya na kuweka kanuni ambayo imeleta solution ambayo nchi nyingi za Afrika zimeshindwa na ndiyo maana dunia ilikuja Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Gwajima kuwa Jemedari tuliye naye nina hakika tuko salama. Ndiyo maana toka mwaka 2022 yeye mwenyewe amekutana na hao wanaofanya tiba hii na kujadiliana na kuanza kuiweka Tanzania kwenye roll kwa ajili ya usalama na mambo mengine.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kweli kwamba kuna mambo yanaweza yakatokea. Kwa mfano, wakati wanaanza kufanya experiment za hili suala katika nchi nne kubwa duniani, mtaalam mmoja wa nchi hizo alitoka Marekani kwenye maabara zinazofanya hii akaenda akakutana na wazazi wenye HIV.
Mheshimiwa Spika, wale wazazi walipokutana, mbegu ya baba na mama ilipokutanishwa basi akaingia kwenye kizazi cha mama akachukua ile mbegu ya mama iliyorutubishwa na mbegu ya baba akaenda maabara halafu aka-edit, akatoa lile eneo la gene linalotoa kile kisehemu kinachosababisha mtu aweze kushika UKIMWI alivyotoa akarudisha kwenye tumbo la mama. Mwisho wa siku wakazaliwa watoto wawili ambao hawawezi kupata UKIMWI hata ukiwawekea ndoo nzima ya damu yenye UKIMWI hawawezi kupata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, mwanasayansi huyo kwenye nchi yake alikamatwa. Inawezekana alikamatwa kwa kufungwa kweli au kwa ajili ya nchi hiyo kuendelea kujifunza hiyo teknolojia zaidi kwa ajili ya kufanya biashara baadaye, lakini nikwambie, ni kweli kwamba lazima tutunge sheria za kuhakikisha tunawalinda wahuni wasifanye chochote kwa kutumia hii teknolojia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, imeshaonekana duniani kuna umuhimu wa kanuni na mambo mengine, lakini hii inahusu gene editing. Mki-edit maana yake unasababisha mtu anabeba mwilini kwako na ataambukiza kwa watoto wake na watoto wake watakuja kuoa watoto wako kwa hiyo hakuna atakaye kuwa salama. Kwa hiyo, yeyote atakayecheza hata na yeye atapata matatizo. (Makofi)

Name

Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza Matibabu ya Wagonjwa Wenye Seli Mundu kwa kutumia Crispr Gene Editing Technology?

Supplementary Question 2

MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi ya swali. Ninampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha huduma hii ya uroto katika Hospitali ya Benjamini Mkapa na kuokoa maisha ya watoto wengi wa kitanzania. Je, ni lini sasa huduma hii itashuka katika Hospitali ya Mkoa wa Mara? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu wakati wote amekuwa mpiganaji muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Mara, lakini nimwambie kwamba Rais wetu amewekeza sana kwenye eneo la teknolojia. Maana yake ili hili liweze kushuka mikoani unahitaji teknolojia na utaalam na tayari Rais wetu kwenye teknolojia ameshawekeza kwenye hospitali zetu na kwenye majengo kwa maana ya hospitali za kanda zinatoa moja.

Mheshimiwa Spika, tukikamilisha hospitali zote za kanda zikawa zinatoa huduma hii, tutaanza kushuka hospitali za mikoa na ndiyo maana unasikia Dr. Samia Specialized Scholarship zile za kwenda kutengeneza Madaktari Bingwa. Ni mkakati maalum wa Rais wetu wa kupeleka madaktari duniani wanakuja na ujuzi mbalimbali na sasa wakija tutakuwa na madaktari, watashuka chini kwa sababu Rais wetu ameshawekeza kwenye eneo la teknolojia. (Makofi)