Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri na kwa yale yote ambayo yanaendelea kufanywa katika jimbo letu la Newala Vijijini, lakini nina masuala mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, suala la kwanza ni ombi, kwa sababu Serikali imeshaahidi kwamba itaenda kufanya tathmini katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ili kubaini na kupanga bajeti. Ombi langu ni kwamba, hiyo tathmini ifanyike kwa haraka ili wananchi wa Newala Vijijini nao wapate huduma zinazostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili ni swali. Kwa dunia tuliyonayo leo, suala la mafunzo ya TEHAMA haliepukiki kwa wanafunzi wetu wote walioko shuleni na tunatambua kwamba zipo shule ambazo zipo katika maeneo ambayo yana changamoto ya mawasiliano, hivyo wanakosa kusoma masomo ya TEHAMA kwa vitendo, wanasoma kwa nadharia. Je, ni upi mpango wa Serikali wa kuwakwamua wanafunzi hawa ili na wenyewe waweze kusoma masomo ya TEHAMA kwa vitendo? Ahsante. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naanza kwa kupokea shukrani, kwa kweli Mkoa wa Mtwara maeneo mengi tayari tumeweza kuyafikia, ni eneo la Mheshimiwa Mbunge la Newala pamoja na Nanyumbu tu, tunaendelea kuja kulifikia.

Mheshimiwa Spika, masuala ya TEHAMA shuleni ni kipaumbele ndani ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa Mradi wa Mkongo wa Taifa. Maeneo mengi tayari mmeweza kujionea namna ambavyo mkongo umeweza kuwafikia na kurahisisha spidi na gharama nafuu ya mawasiliano ya data kwa maana ya internet.

Mheshimiwa Spika, shuleni, kwa mpango wa Serikali tutafikisha huduma hii ya Mkongo wa Taifa. Hivyo nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba maeneo ya Newala Vijijini pia tunatarajia kufikia Desemba 2025 iwe imeweza kufikiwa.

Mheshimiwa Spika, vilevile, kwa mawasiliano kwa ujumla maeneo ya mipakani ninafahamu usikivu wa redio unakuwa ni tatizo. Mheshimiwa Mbunge tumeshaongea mara nyingi katika hili, nikutoe hofu, TBC FM pia mtakuja kufikishiwa na usikivu utakuwa imara kabisa. Mtaacha kusikiliza redio za jirani na kusikiliza redio yetu ya TBC FM na nyingine nyingi.

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 2


MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katika Kata za Kiteto zenye changamoto ya mawasiliano zikiwepo Kata za Makame, Ndedo na Njoro?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer


NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kuhusu minara ya Kiteto, kazi zinaendelea. Nimtoe hofu Mheshimiwa Rahhi kwamba tuendelee kuvuta subira. Ninaamini watoa huduma wetu wote wataendelea kukamilisha minara hii kwa wakati, ahsante. (Makofi)

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 3

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili kuuliza swali dogo la nyongeza. Kata ya Tangazo, Naumbu, Kijiji cha Namgogoli, hakuna kabisa minara ya mawasiliano. Je, ni lini Serikali itapeleka minara ya mawasiliano katika maeneo hayo? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, kata hizi zote alizozitaja Mheshimiwa Shamsia ziko katika mpango wa kuhakikiisha wanajengewa minara kwa lengo la kupata mawasiliano ya uhakika. Kwa hiyo, tukishindwa kwa mwaka huu wa fedha, mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuwafikia. (Makofi)

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 4

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ni takribani miaka miwili toka nimeomba mnara katika Kata ya Uru Kusini na hadi leo hatujapatiwa. Je, ni lini sasa tutawekewa mnara katika kata hiyo ili tuache kukaa kwenye miti kupiga simu? Ahsante. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, suala la kata hii aliyoitaja Mheshimiwa Shally Raymond, naomba niwe nimelipokea na kwenda kulifanyia kazi kuona wamefikia hatua gani? Ahsante. (Makofi)

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 5

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nami nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Serikali ilikuwa na mkakati wa kujenga mnara wa mawasiliano katika Kata ya Uru Kusini ambapo hakuna mawasiliano kabisa, na mkakati huu ulisitishwa.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, kata hizi zote zimeshafanyiwa tathmini na kazi ya tathmini inaendelea. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Njau, kadiri tunavyoendelea kupata fedha tutaendelea kuhakikisha maeneo haya yote wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika kwa ujenzi wa minara, ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, kata zetu zilizo mpakani na nchi mnayoifahamu, mawasiliano yake yanaingiliwa sana na mawasiliano kutoka kwenye nchi hiyo na hatupati signals kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Kata za Kirua Vunjo Magharibi, Marangu Magharibi, Kilema Kaskazini, Mamba Kaskazini na Mwika Kaskazini hazina mawasiliano mazuri kabisa. Kwa hiyo, tulikuwa tunatarajia kwamba ule mgao wa minara wa awamu ya pili tungepata minara. Je, ni lini mgao huo utafanyika? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Dkt. Kimei kwamba maeneo yote ya mipakani tayari tumeweka mpango maalumu na mahususi kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanakuja kujengewa minara ili waweze kupata mawasiliano ya ndani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hata kwenye usikivu wa redio, tayari tuko kwenye mkakati wa kuhakikisha maeneo yote ya mipakani wanaacha kusikiliza redio kutoka nchi za nje na waendelee kupata usikivu kutoka redio zetu za ndani. Kwa hiyo, tayari kama Wizara tunaendelea kulifanyia kazi.

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 7

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Hali ya usikivu wa Redio yetu ya TBC katika Wilaya ya Kishapu ni ya chini sana. Sasa, nataka niulize swali, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba wananchi wa Kishapu wanaendelea kupata taarifa za uhakika kutoka TBC katika kipindi hiki cha mwaka huu? Ahsante. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Boniphace Butondo, Mbunge wa Kishapu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu usikivu wa TBC FM kuwa chini, naomba niwe nimelipokea ili tuwasimamie wataalamu wetu waje kuona namna ya kuuboresha mnara huo na mawasiliano ya TBC FM yaweze kupatikana vizuri kabisa. (Makofi)

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 8

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, Serikali ilituahidi katika awamu ya kwanza minara 700 na zaidi kujengwa katika Kijiji cha Kintanula, Kata ya Mwamagembe, Halmashauri ya Itigi, ni lini mnara huu utajengwa? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, minara hii 758 utekelezaji unaendelea. Katika eneo hili la Itigi kijiji alichokitaja Mheshimiwa Massare nalo tutalifuatilia kuona wapi imekwama ili tuweze kutoa msukumo na mnara huu uweze kujengwa ndani ya wakati. Ahsante.

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 9

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itajenga minara ambayo tuliiomba kwenye eneo la Getanyamba, Changanyikeni, Mewadan, Haydarer na Endahagichan na Qamtananat? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Flatei Massay kwa kweli yote yapo katika mpango na tutahakikisha tunaendelea kuyatekeleza na kusimamia watoa huduma wote waliosaini mikataba wakajenge minara hii.

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 10

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kata za Ntaba, Kambasegela, Kabula pamoja na Mpata zina changamoto kubwa sana za kimawasiliano. Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini mtapeleka mawasiliano katika kata hizi? Ahsante.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fredy Mwakibete, Mbunge wa Busokelo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, haya maeneo aliyoyataja Mheshimiwa Mwakibete na yenyewe pia tutaendelea kuyapa kipaumbele kuona minara inakuja kujengwa na kuimarisha mawasiliano.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 11

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Matwebe katika Jimbo la Rungwe kumekuwa hakuna kabisa mawasiliano ya simu mpaka uende kwenye sehemu za miinuko. Ni lini Serikali itapeleka minara maeneo hayo? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, eneo hili la Matwebe na lenyewe pia, tunatamani Tanzania nzima na ndiyo maana tukaweka ile minara 758. Tuna minara 636 na tuna project nyingi ambazo tayari zipo katika mpango.

Mheshimiwa Spika, napenda tu kusema, nchi nzima tutakwenda kuifikia na kuona kwamba mawasiliano yanaimarishwa. Kwa hiyo, minara hii ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge itajengwa. Nawaomba tu kuwa na subira na mwendelee kutuunga mkono. Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari tuna nia njema ya kuhakikisha maeneo yote nchini tunakwenda kuimarisha mawasiliano.

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Supplementary Question 12

MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Micheweni usikivu wa TBC FM ni mdogo sana. Je, Mheshimiwa Waziri ni lini nasi utatujengea mnara katika Wilaya ya Michweweni ili kuwawezesha wananchi kuisikiliza redio yao? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, nafikiri ni miezi miwili tu imeisha toka nimeweza kufanya ziara Zanzibar. Nimeacha maagizo maeneo haya yote yaweze kushughulikiwa. Hivyo na eneo hili la Micheweni naomba niseme nimelipokea kwa ufuatiliaji zaidi. (Makofi)