Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omar Issa Kombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 1
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, uhai wa Bunge la 12 unaenda kwisha sambamba na mwaka wa fedha husika, mpaka sasa katika kituo chetu hakuna mkandarasi wala hakuna shughuli yoyote inayoendelea tunaomba commitment ya Serikali ni lini kituo hiki kinaanza kujengwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kipenzi cha Wazanzibari Mheshimiwa Rais Hussein Ally Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amepeleka miradi ya kutosha katika Wilaya yetu ya Micheweni. Je, Serikali hamwoni ni muhimu kupeleka nguvu ya ziada katika ujenzi wa mradi huu? Ahsante.
Name
Cosato David Chumi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Omar Issa Kombo Mheshimiwa Mbunge wa Wingwi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi commitment ya Serikali ni kwamba katika mwaka huu wa fedha 2024/2025, tunaanza kujenga ujenzi huu. Kwanza tulitenga fedha kwa ajili ya kukarabati jengo lililopo, lakini baada ya kufanya tathmini tukaona jengo limechakaa kabisa halifai kukarabatiwa, ndiyo maana sasa tumeongeza fedha kwa ajili ya kuanza kujenga Kituo Kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba kule Zanzibar kazi kubwa imefanyika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba nguvu hiyo hiyo iliyotumika kukamilisha miradi mingine pia itatumika kuhakikisha kwamba Kituo cha Polisi Wilaya ya Micheweni pia inakamilika kwa wakati. Ahsante sana.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilitenga bajeti ya shilingi milioni 115 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kipatimo mwaka huu wa fedha. Je, ni lini fedha hizo zitafika kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho? Ahsante sana.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Francis Ndulane, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwenye mwaka wa fedha 2024/2025, tulitenga fedha milioni 115 kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Kipatimo ambacho kipo kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge. Mwaka wa fedha unaendelea na Serikali ipo kazini, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge fedha zitaenda kama zilivyoenda hizi zingine kwa ajili ya kumalizia Kituo cha Polisi alichokitaja. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 3
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilituahidi kujenga Kituo cha Polisi Kata ya Rundugai kwa sababu wananchi wanatembea umbali mrefu sana kufata huduma Kituo cha Polisi Bomang’ombe ni lini ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Rundugai utaanza? Ahsante.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu la nyongeza ya Mheshimiwa Mafuwe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumepanga kujenga ujenzi na Vituo vya Polisi vya Kata na Sheia kwa upande wa Zanzibar awamu kwa awamu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, nia ya Serikali ni kuhakikisha kila Kata ya nchi hii inapata Kituo cha Polisi kama ambavyo tayari tumeshapeleka askari katika maeneo hayo. Mheshimiwa Mbunge Serikali itatenga fedha na kujenga kituo cha polisi ulichokijenga kwenye Wilaya ya Hai. Ahsante sana.
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 4
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kukikarabati Kituo cha Polisi cha Maturubai ambacho kinahudumia wakazi wengi wa Jimbo la Mbagala?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Abdallah Chaurembo Mheshimiwa Mbunge wa Mbagala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya Polisi vya Kata pamoja na Wilaya kama ambavyo ameuliza Mheshimiwa Mbunge. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kituo chake alichokisema cha maturubai tutakichukua tutakiweka kwenye mpango na kukitengea fedha kwa ajili ya kukifanyia ukarabati ili aweze kutoa huduma kwa wananchi wa Mbagala. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved