Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dua William Nkurua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. DUA W. NKURUA aliuliza:- Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne alitoa ahadi Mkoani Mtwara ya kumaliza tatizo la maji katika Mji wa Mangaka kwa kuchukua maji kutoka Mto Ruvuma, mradi ambao pia ungeweza kutatua tatizo la maji katika vijiji zaidi ya 12 vitakavyopitiwa na bomba kuu la mradi huo:- Je, utekelezaji wa ahadi hiyo umefikia wapi?

Supplementary Question 1

MHE. DUA W. NKURUA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri na yanayotia moyo kwa wananchi wangu wa Nanyumbu.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Nanyumbu tulikuwa na bahati mbaya ya gari la Programu ya Maji kupata ajali, gari ambalo sasa haliwezi kutumika kabisa.
Je, Mheshimiwa Waziri ana mpango gani sasa kuipatia Wilaya ya Nanyumbu gari ili wataalam waweze kutoa huduma hizo kwa wananchi?
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ingawa swali hili limepata majibu kidogo hafifu kutoka kwa Mheshimiwa Nkamia, lakini nataka pia tuna tatizo la wakandarasi kuzidai Halmashauri pesa za maji za Benki ya Dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini hasa tutawalipa hawa Wakandarasi ili kuondokana na kero ya mgogoro kati ya Halmashauri na Wakandarasi hao? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la gari ambalo limeharibika, tutaliangalia na tutakapopata fedha tutalifanyia matengenezo na kama matengenezo yatashindikana, basi tutafanya utaratibu wa kununua gari lingine jipya ili wananchi wa Mangaka waendelee kupata huduma ya maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kabisa kwamba kuna miradi mingi ambayo imechelewa kukamilika kwa sababu ya fedha zinazoitwa fedha za Benki ya Dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na matatizo ya kifedha katika nchi ambayo yamesababisha miradi mingi ya maji isikamilike. Hata hivyo, tunamuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kuanzia sasa fedha zinaanza kutolewa ambazo zitahakikisha kwamba miradi yote ambayo ilikuwa haijakamilika, inakamilika pamoja na miradi ya Mheshimiwa Mbunge.