Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo wadogo imekuwa ikitoa ruzuku ili kuwawezesha wachimbaji kunufaika na madini yapatikanayo maeneo mbalimbali nchini:- (a) Je, mpango huo umenufaisha wachimbaji wangapi nchini? (b) Je, ni Mikoa na Wilaya zipi zinazonufaika na mpango huo? (c) Je, Serikali ipo tayari kuweka utaratibu wa kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo ili kuwawezesha kuchimba madini?
Supplementary Question 1
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na nia na dhamira nzuri ya Serikali juu ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo lakini imeonekana kwamba masharti haya hayawasaidii hawa wachimbaji wadogo na tunajua kwamba sasa hivi wimbi kubwa la watu wanaokosa kazi ni vijana. Sasa, je, Serikali iko tayari kupunguza vigezo vile ili watu wengi waweze kunufaika na mpango huu?
Swali langu la pili, je, Naibu Waziri yupo tayari kuambatana nami kwenda Jimboni ili tuweze kuzungumza na wachimbaji wadogo ili wajue dhamira ya Serikali ya kuwasaidia hususan wachimbaji wadogo? Ahsante.
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Kigua kwa kutambua kwamba kulikuwa na vikwazo tulipoanza utaratibu huu. Tumepunguza vikwazo vya kuomba mikopo. Tulipoanza kutoa ruzuku mwaka 2013 ilikuwa siyo ruzuku, ilikuwa ni mikopo. Sasa Serikali imepunguza masharti ya mikopo na badala yake sasa inatoa ruzuku. Hilo ni jambo muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kikwazo cha pili kilikuwa ni lazima wachimbaji wawe na Bankable statement inayoonyesha rasilimali ya madini iliyoko hapo chini. Sasa kulingana na uwezo mdogo wa wachimbaji wadogo, kigezo hicho kimeondolewa. Kwa hiyo, tunashukuru Mheshimiwa na vigezo vinaendelea kupungua ili Watanzania wengi wanufaike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niko tayari kutembelea kwenye Jimbo la Kilindi na hasa maeneo ya Tunguli. Ningependa nifike Tunguli lakini hata Kwa Manga mpaka kule kwenye Kijiji cha Kikunde na Mafulila ambako wanachimba wachimbaji wengi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved