Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

CAN.RTD Ali Khamis Masoud

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mfenesini

Primary Question

MHE. KANALI (MST.) MASOUD ALI KHAMIS (K.n.y MHE. IBRAHIM HASSANALI MOHAMMEDALI) aliuliza:- Serikali imeanzisha mabasi yaendayo kwa kasi katika Jiji la Dar es Salaam lakini madereva wengi wamekuwa wakiendesha magari hayo kwa kasi kubwa; kiasi cha kuhatirisha maisha ya watu waendao kwa miguu. (a) Je, ni lini Serikali itawachukulia hatua madereva ambao hawafuati Sheria za Barabarani? (b) Je, ni muda gani magari hayo ya DART yamepangiwa kuanza kazi na kuda wa kumaliza kazi?

Supplementary Question 1

MHE. KANALI (MST.) MASOUD ALI KHAMIS : Mheshimwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nilikuwa naomba kuuliza swali la nyongeza.
Je, mabasi haya yana idadi maalum ya kupakia abiria na kama hayana idadi ni kwa nini?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwanza tuna mabasi ya aina mbili, yale mabasi marefu zaidi na mabasi mafupi, na mabasi haya kila basi lina idadi yake.
Kwa hiyo, nimuondoe shaka Mheshimiwa Mbunge, mabasi haya yana idadi maalumu isipokuwa wakati mwingine katika vituo mabasi yakifika watu huwa wanakimbizana kuingia ndani ya mabasi.
Mheshimiwa Spika, utaratibu umewekwa kuhakikisha kuwa watu wanapanda mabasi hayo kwa kuzingatia idadi yake ili kulinda usalama wa raia katika suala zima la usafiri.