Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Martin Alexander Mtonda Msuha
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Vijijini
Primary Question
MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:- Wananchi wa Mbinga wanaishukuru Serikali kwa mradi wa kusambaza umeme vijijini kwani wana imani mradi huo utasaidia kuinua hali za maisha. Hata hivyo ni vijiji 34 tu ndiyo vimepatiwa umeme kupitia mpango wa usambazaji umeme unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili. Je, lini Serikali itapeleka umeme katika vijiji 118 vilivyosailia?
Supplementary Question 1
MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Spika, asante pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, mpango wa REA III una-cover mwaka 2016 mpaka 2019/2020. Serikali ina mpango gani kushirikisha Waheshimiwa Wabunge katika kupanga maeneo ya kupeleka umeme katika miaka hiyo husika kuzingatia kwa bajeti ya kila mwaka?
Mheshimiwa Spika, swali la pili Mkoa wa Ruvuma haujaunganishwa bado na umeme wa Gridi ya Taifa. Ni lini sasa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Makambako kwenda Songea utakamilika?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, nishukuru kabisa Mheshimiwa Mbunge ametukumbusha kwamba tuwaambie Waheshimiwa Wabunge. Kwanza kabisa niwaondoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge, mradi wa REA Awamu ya Tatu unaoanza sasa tunatumia utaratibu ufuatao:-
Mheshimiwa Spika, wakandarasi watakapokuwa wanaingia site kuanzia Disemba mwaka huu, hatua ya kwanza itakuwa ni kukutana na kukubaliana na Waheshimiwa Wabunge kabla hawajaanza kazi kwenye maeneo yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini nitoe tu angalizo lingine, kwamba tumeweka utaratibu sasa mahali ambako kuna Ofisi zetu za TANESCO tumeandaa kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali za Mitaa kuweka vituo rasmi ili wananchi wasiende kwenye Ofisi za TANESCO ila wafanyakazi wa TANESCO wakae kwenye vituo ambavyo Serikali za Mitaa zitakuwa zimetambua.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wabunge pamoja na Diwani watashirikishwa sana kabla ya utekelezaji wa mradi huu kuanza.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mradi wa Makambako – Songea, mradi wa Makambako – Songea una sehemu tatu za utekelezaji. Sehemu ya kwanza ni ujenzi wa distribution line ambao inachukua urefu wa kilomita 900 kwa maeneo yote ya Mbinga, Songea na maeneo mengine.
Mheshimiwa Spika, mradi huu ulianza mwaka juzi na unakamilika mwakani mwezi Julai. Sehemu ya pili ni kujenga transmission line ambayo imeanza mwaka jana na hivyo itakamilika mwezi Septemba, 2018. Hatua ya tatu ni kujenga substations tatu, moja ikiwa Makambako, nyingine Songea na nyingine eneo la Madaba, kwa ujumla wake kazi zote zitakamilika mwezi Mei, 2018.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved