Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Wilaya ya Maswa ni moja ya Wilaya kongwe hapa nchini, lakini haina kituo cha Polisi cha Wilaya:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi cha Wilaya.
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza kabisa namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya kuridhisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Kituo cha Polisi cha Maswa ni cha muda, kiko kwenye hifadhi ya barabara ambapo kinaweza kikabomolewa wakati wowote ili kupisha ujenzi wa barabara; je, ni lini Serikali itajenga kituo cha kudumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa vile tatizo lililoko Wilaya ya Maswa liko sawa kabisa na tatizo lililoko Wilaya ya Itilima, hakuna kituo cha Polisi cha Wilaya; je, ni lini Serikali itajenga kituo cha Polisi cha Wilaya ya Itilima?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Esther alitaka kujua ni lini Serikali itajenga kituo cha Polisi Itilima pamoja na Kituo cha Kudumu Maswa. Naomba nimjulishe Mheshimiwa Esther kwamba kama nilivyojibu katika swali langu la msingi ni kwamba tunatambua upungufu wa vituo 65 nchi nzima katika Wilaya 65 ikiwemo Maswa na Itilima. Kwa hiyo, pale ambapo tutafanikiwa kupata fedha za ujenzi huu tutatoa kipaumbele katika maeneo hayo kama ilivyo maeneo mengine ya Wilaya zilizobakia 65 ambazo hazina vituo vya Polisi mpaka sasa hivi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved