Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdulaziz Mohamed Abood
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Mjini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Maeneo mengi katika Jimbo la Morogoro Mjini bado hawajapata nishati ya umeme kama vile Kata za Mindu, Lugala, Mkundi, Kiegea A na B, Kihonda, Mafisa, Tungi, Kingolwira na Kauzeni A. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo hili la muda mrefu?
Supplementary Question 1
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Morogoro inaelekea kuwa Jiji, je, Serikali ina mikakati gani ya kumaliza maeneo yote ya Mji wa Morogoro kuwa na umeme?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna maeneo ambayo umeme umeshafika, wananchi wameshalipia kuunganishiwa umeme, lakini majibu wanayopewa ni kuwa nguzo hakuna. Je, Serikali itaondoa lini kero hiyo ya nguzo katika Mji wa Morogoro ili wananchi waweze kupata umeme, maeneo waliyokwishapata umeme?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali kupeleka umeme ni kama ambavyo nimeeleza, ipo miradi ya REA, lakini pamoja na REA bado TANESCO wana bajeti zake za kupeleka umeme. Katika Mkoa wa Morogoro, hasa Morogoro Mjini, mkakati uliopo wa kwanza kabisa, Serikali imetenga shilingi milioni 106 kwa mwaka huu ambayo itapeleka umeme kwenye vijiji vya Mheshimiwa Abood ikiwemo Kihonda, Mafisa pamoja na maeneo mengine kama kule Kanisani ambako ameeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine ambayo Mheshimiwa Mbunge hajayataja pamoja na eneo lake lile ambalo amesema eneo la Bomba la Zambia. Kile Kijiji cha Bomba la Zambia ambacho kipo mbali sana kitapelekewa umeme mwaka huu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Abood kwamba Serikali ina mkakati madhubuti wa kupeleka umeme kwenye vijiji vyake vyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili kuhusiana na nguzo, ni kweli kabisa yako maeneo Morogoro Mjini wananchi wamelipia, lakini hawajawahi kuunganishiwa umeme. Utaratibu unafanyika sasa na nimhakikishie Mheshimiwa Abood hivi sasa tunapoongea hapa wananchi wake wa Lokole Juu pamoja na Lukobe Kanisani wanaunganishiwa umeme kwa sababu wameshalipia na nguzo zimeshakuja na vijiji vinne ambavyo amevitaja pamoja na Kauzeni na maeneo mengine wataendelea kuunganishiwa umeme mara baada ya nguzo kuingia mwezi ujao.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved