Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Janet Zebedayo Mbene
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ileje
Primary Question
MHE. JANET Z. MBENE aliuliza:- Jumuiya za kiuchumi za Kikanda zimekuwa sehemu ya mkakati mkubwa katika kuratibu masuala ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimazingira. Ileje ni Wilaya ya mpakani mwa Nchi za Malawi na Zambia lakini haina kituo cha forodha. Hakuna miundombinu ya soko la Kimataifa, hakuna kituo cha uhamiaji, hakuna kituo cha kudhibiti mazao, mifugo wala silaha. Hii inasababisha wahamiaji haramu na wahalifu kutumia mipaka kinyume cha sheria na taratibu:- Je, ni lini Serikali itajenga kituo cha forodha, kituo cha uhamiaji, soko la Kimataifa na kituo cha kukagua mifugo na silaha kwa ufanisi na maendeleo ya Ileje?
Supplementary Question 1
MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutupa moyo na kutuhakikishia kuwa tayari mikakati ya kutuwekea kituo cha forodha iko njiani. Hata hivyo, nataka vilevile nimtake
Mheshimiwa Waziri na Serikali kuharakisha mipango hiyo kwa sababu hivyo vituo vya jirani anavyovizungumza bila shaka anazungumzia Kasumulo iliyopo Kyela, anazungumzia Tunduma ambavyo vyote viko mbali sana na Ileje na Ileje
kama inavyofahamika hakuna barabara hata moja
inayopitika vizuri, kwa hiyo kutuambia sisi twende tukatumie vituo vile ni kama kutudhihaki. Pamoja na hayo, tayari ardhi imeshaanza kupimwa na inamaliziwa, tayari maeneo yameshaainishwa, tayari wahusika wameshakuja kukagua maeneo, namwomba sasa Mheshimiwa Waziri anihakikishie
kuwa sasa hatua itakayofuata ni ujenzi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Malawi; Malawi
tayari wana kituo, wanatungojea sisi. Miundombinu yetu sisi ndiyo inachelewesha kile kituo cha Malawi kushirikiana na cha kwetu. Kwa hiyo, naomba sana hilo lifahamike na
atuhakikishie hapa ni lini sasa hatua hizo zitafanyika? Ahsante sana.
Name
Dr. Philip Isdor Mpango
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumthibitishia Mheshimiwa Mbunge Janet Zebedayo Mbene, Mbunge wa Ileje kwamba maoni yake yatazingatiwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved