Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Tanzania ni nchi yenye misitu mingi na Sheria ya Usafirishaji wa Mazao ya Misitu inazuia kusafirisha zaidi ya sentimeta15 au inchi sita. Je, Serikali imepata hasara kiasi gani kwa kuruhusu usafirishaji wa sentimeta 20 sawa na inchi nane ili kujenga uwezo wa kiushindani na nchi nyingine katika soko?
Supplementary Question 1
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii, pia nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Lakini pamoja na majibu hayo mazuri nina maswali madogo tu ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ya Maliasili kupitia TFS imekuwa ikitoa vibali vya kuvuna mazao ya misitu. Mvunaji anaanzia vijijini, Wilayani kwenye kanda na hadi Wizara, lakini kabla ya kuruhusiwa kuvuna mazao ya misitu, Serikali imekuwa ikiwasajili wadau hawa na kuwatoza pesa kila mwaka. Vilevile kumekuwepo na tatizo kubwa la Wizara hii kuwa ikishatoa vibali hivi inachukua muda mfupi tu kuvifuta kama ilivyokuwa mwaka huu ambapo vilitolewa vibali zikiwemo approval za…
… kutoka nchi za nje na baadae vilifutwa na Mheshimiwa Waziri, sasa swali.
(a) Je, ni lini Serikali itaacha utaratibu huu mbaya na ambao unawatia hasara wadau wao?
(b) Serikali haioni sasa ni vyema isitoe approval hizi hadi ijiridhishe kwamba wananchi na wadau hawa wakipewa vibali hivyo watafanya kazi kwa mwaka mzima kuliko kama hivi wanatoa na kufanya kazi kwa miezi miwili tu na kuwasimamisha?
Name
Eng. Ramo Matala Makani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi suala la uvunaji wa maliasili linatokana na ukweli kwamba nia na dhamira ya Serikali ni kuliwezesha Taifa hili kuweza kutekeleza mipango yake yote ya maendeleo kwa kutumia rasilimali za Taifa hili ikiwemo maliasili. Jambo la msingi ni kwamba tunatakiwa kutumia maliasili hizo kwa namna ambayo ni endelevu. Kwa hiyo, udhibiti haumaanishi kwamba rasilimali hizi au maliasili hizo zisitumike kabisa, hapana, nia ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunafanya matumizi endelevu ili tuweze kuendana hata na malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuhusu swali lake moja kwa moja la utaratibu wa utoaji wa vibali, huo ni utaratibu ambao utatuwezesha kutoa fursa kwa kila mwananchi ya kuweza kushiriki katika uvunaji wa raslimali hizo. Lakini ikiwa kwamba, utaratibu huo unaonekana pengine una kasoro basi kwa kuwa ulikuwepo kwa mujibu wa sheria basi…
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anayo fursa ya kufuata utaratibu wa kawaida wa kuleta maoni ili tuweze kupitia upya sheria hiyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved