Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Alex Raphael Gashaza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Maporomoko ya maji ya Rusumo yanapatikana katika Jimbo la Ngara nchini Tanzania na Wilaya ya Kirehe nchini Rwanda kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda na maporomoko haya yanaweza kuwa kivutio kizuri cha kitalii. Je, Serikali iko tayari kufanya utafiti katika eneo hili ili liweze kurasimishwa kwa ajili ya shughuli za kitalii ili kuongeza pato la Wilaya na Taifa kupitia sekta hiyo ya utalii?

Supplementary Question 1

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri na ambayo yanatia matumaini. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kutambua kwamba kuna vivutio hivyo katika Jimbo la Ngara, kama maporomoko hayo, lakini bado hifadhi hizo za Burigi na Kimisi na bado kuna vivutio vingine kama pango lililokuwa linasafirisha watumwa kutoka Burundi kupitia Tanzania, pango la Kenza Kazingati, kuna mlima mrefu kuliko milima yote Mkoa wa Kagera, kuna mito miwili ambayo unaweza ukafanya boat riding na ili vivutio hivi kufanya kazi na kupata watalii ni lazima kuboresha miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege, sasa tuna uwanja wa ndege wa Luganzo. Je, Wizara iko tayari kuboresha uwanja huu wa ndege wa Luganzo ambao unaweza ukasaidia kuleta watalii na wakafanya utalii katika eneo hilo? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilitegemea kupata gawio la asilimia 25 kutokana na utalii wa uwindaji katika Hifadhi za Burigi na Kimisi. Hata hivyo, takribani miaka 30 iliyopita tangu Hifadhi ya Burigi imeanzishwa na miaka takribani 12 tangu Hifadhi ya Kimisi imeanzishwa ni mwaka jana tu ambapo tumeweza kupata gawio la shilingi milioni 7, gawio ambalo ni dogo. Sasa nahitaji nipate ufafanuzi kwamba shilingi milioni 7 hizi zilitokana na mapato ya kiasi gani na ni wanyama kiasi gani waliowindwa katika hifadhi hizi mbili? (Makofi)

Name

Prof. Jumanne Abdallah Maghembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Gashaza kwa ufuatiliaji wake wa karibu na mawazo mazuri katika kuendeleza na kuboresha maeneo haya kama maeneo yanayovutia watalii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna uwanja wa ndege ambao umekuwa unatumiwa na wawindaji katika eneo lile ambao urefu wake ni mita 1,700. Tutatuma wataalam wetu wanaoshughulika na masuala ya uwindaji ili washirikiane na TAA katika kuboresha uwanja huu ili kuhakikisha kwamba vivutio hivi vinaweza kufikiwa kwa urahisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la uwindaji, Wizara yangu itafuatilia zaidi malipo ambayo yamefanywa ili kuona ni namna gani tunaweza kuboresha ushirikiano kati ya wawindaji, Wizara na wananchi wa Ngara, ili kuboresha hali ya uwindaji katika eneo hilo.