Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Julius Kalanga Laizer
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Monduli
Primary Question
MHE. JULIUS K. LAIZER aliuliza:- Mheshimiwa Rais alipokuwa anaomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015 aliahidi kuwa Serikali itakarabati mabwawa matatu ya josho, mto Mbu na Olkuro:- (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hiyo ili wananchi wa Esilalei waweze kupata maji kwa ajili ya mifugo yao? (b) Je, ni lini Serikali itawapatia wananchi wa Sepeko na Lepurko maji safi na salama?
Supplementary Question 1
MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitumie fursa hii pia kuishukuru Serikali kwa kutuongezea matenki mawili ya maji katika Kata ya Nalalami na Moita.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, kwa kuwa mradi huu kweli umeanza katika Kata ya Sepeko katika Kijiji cha Lendikinya lakini mradi huu umesimama karibu miezi miwili na miradi mingine minne katika Jimbo la Monduli kwa sababu ya upatikanaji wa fedha ambapo wakandarasi wameandika barua ya kusimamisha mradi na hakuna kazi yoyote inayoendelea kwa sababu Serikali imeshindwa kulipa fedha kwa wakati kwa wakandarasi. Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu kulipa fedha za wakandarasi ili waweze kurudi site na kuendelea na mradi kwa ajili ya kuwapatia wananchi maji katika kipindi hiki ambacho kiangazi kimeanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa tatizo la maji na lenyewe limeendelea kuwa kubwa nchini ni lini Serikali itafanya utafiti wa kutambua ukubwa wa tatizo kwa kila halmashauri katika nchi yetu ili kuleta mipango thabiti ya kuwapatia wananchi maji, kuliko ahadi hizi ambazo zinachua muda kukamilika?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS - TAMISEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nipokee hii concern kwamba certificate zimeenda lakini bado hazijalipwa. Naomba niweke kumbukumbu sawa; juzi nilitoka Malinyi nilikutana na mradi mkubwa wa maji ambapo tulipata concern kama hiyo. Kwa kushirikiana na Wizara ya Maji tutaziangalia zile certificate ambazo wakandarasi wameshapeleka ambazo zinahitaji malipo zifanyike kwa haraka. Lengo kubwa ni kuwa wakandarasi waendelee na miradi ili ikamilike na wananchi waweze kupata maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kufanya utafiti katika halmashauri zote; nakumbuka, tukifanya rejea katika Bunge la Bajeti, nilizungumza na kuziagiza halmashauri zote zifanye tathmini ya miradi yote inayotengenezwa kwa sababu tunaona kwamba tuna idle project maeneo yote ya nchi na nilitoa deadline siku ile nikiwa hapa Bungeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati nzuri tumeshapata tathmini ya nchi nzima ya miradi yote nini kimekwamisha. Lengo letu ni kujua changamoto zinazoikabili miradi ya maji na nini tufanye. Kwa hiyo mpango huo Mheshimiwa Julius tumeshaenda mbele zaidi, tumeshafanya hilo. Ofisi yetu pale sasa hivi kupitia team ya ma-engineer wetu wanafanya kazi kubwa ya kufanya uchambuzi na kuweka mikakati ambayo italeta majibu ya kuhakikisha miradi hii tunaiwekea mipango sahihi ya kuweza kuitekeleza ili wananchi waweze kupata huduma ya maji kama tunavyokusudia.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved