Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Shamba la Kampuni iliyokuwa ikiitwa Tanganyika Packers lenye ekari 45,000 katika Halmashauri ya Itigi limetelekezwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata nne (4) na vijiji 12 wamekuwa wakilitumia kwa kilimo na ufugaji:- (a) Je, ni lini Serikali itapendekeza kwa Mheshimiwa Rais kufutwa kwa hati hiyo? (b) Je, ni lini Serikali italirudisha rasmi shamba hilo kwa Halmashauri ya Itigi ili lipangiwe matumizi kwa ajili ya wakulima na wafugaji?
Supplementary Question 1
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali madogo mawili:-
Kwa kuwa, dhamira ya Serikali hii ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha wananchi wake wanajitegemea hasa katika suala la chakula, pia kuhakikisha wananchi hawavamii hifadhi zilizotengwa kwa ajili ya kuhifadhi wanyama na misitu ya hifadhi. Pia kwa kuwa eneo langu la Itigi eneo wananchi ni asilimia 35 tu, asilimia 65 ni eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya hifadhi ya Wanyamapori ya Rungwa, Muhesi na maeneo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, shamba hili ndiyo shamba lenye rutuba na ndiyo shamba ambalo lina kiwango kizuri cha kufanya wananchi waweze kunufaika na kujitegemea kwa chakula na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo alipokuja Itigi katika mkutano wake wa hadhara na wananchi aliwaambia na kuwahakikishai wananchi kwamba shamba hili sasa litarudishwa kwa wananchi;
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo na shamba hili liko kwenye Wizara ya Kilimo, aliwadanganya wananchi wa Itigi kwamba atawarejeshea shamba hili?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Kampuni hii ya Tanganyika Packers ilishafilisika, haipo kisheria na ilishafutwa, je, sasa Serikali iko tayari kutekeleza yale ambayo Mheshimiwa Rais alipokuja Itigi alisema kwamba atawasaidia wananchi wa Itigi shamba hili ili liwanufaishe jamii nzima?
Name
William Tate Olenasha
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa nilipofika Itigi nilitoa ahadi kwamba Serikali itachukua hatua kuhakikisha kwamba shamba analolizungumzia litarudi kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimfahamishe Mbunge kwamba utaratibu huo umeshaanza kwa sababu Wizara ambayo awali ndiyo ilikuwa inamiliki hilo shamba imeshawasilisha taarifa kwa Treasury Register ili utaratibu wa kurudisha utaratibu kwa wananchi na hasa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi iweze kufanyika. Kwa hiyo, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba siyo uwongo, hatukudanganya lakini mchakato unaendelea.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved