Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Katika Jimbo la Tunduru Kusini kuna vituo vitatu vya afya. Kituo cha Afya Mtina kina zaidi ya miaka 30 hakijafanyiwa ukarabati na pia hakuna wodi ya wazazi. Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika kituo hicho na kufanya ukarabati ili kiweze kutoa huduma bora kwa wakazi wa vijiji vya Nasya, Semeni, Nyerere, Angalia na wakazi wa kata ya Mchesi na Lukumbule?
Supplementary Question 1
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu aliyotoa Naibu Waziri, lakini Jimbo langu la Tunduru Kusini vituo vyake vya afya vimechakaa na vina hali mbaya na vina matatizo lukuki pamoja na uhaba wa wafanyakazi,hakuna gari, wala chumba cha upasuaji.
Swali langu, ni lini Serikali itahakikisha vituo hivi vya afya vinapata watumishi wa kutosha ili viweze kuhudumia wananchi wa Tunduru?
Swali la pili, katika kampeni ya uchaguzi mwaka 2010, Rais wa Awamu ya Nne alitoa ahadi ya kujenga kituo cha afya katika Mji wa Nalasi ambao una zaidi ya watu 25,000. Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hii ya kujenga kituo cha afya pale Nalasi ili kuweza kuwahudumia wananchi wale ambao wako katika vijiji sita katika Mji ule wa Nalasi? Ahsante.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, katika suala zima la kuongeza watumishi, Serikali hivi sasa iko katika mchakato wa kuajiri watumishi mbalimbali. Katika hilo Jimbo la Tunduru tutalipa kipaumbele katika suala zima la mgawo wa watumishi kwa sababu Tunduru ina changamoto kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, eneo la pili nashukuru Mheshimiwa Mpakate alini-accompany vizuri sana wakati nimeenda katika Jimbo lake. Ni kweli watu wasioijua Tunduru, ukitoka barabarani mpaka Jimbo la Mheshimiwa Mpakate kuna changamoto kubwa sana. Ndiyo maana Mheshimiwa Mbunge alipoleta request, tukaamua kipaumbele cha kwanza twende tukamjengee kurekebisha Kituo cha Afya cha Mkasare.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba leo ninavyozungumza tayari tumeshaingiza shilingi milioni 500 kwa ajili ya kituo kile. Katika kituo kile tutajenga jengo la upasuaji, mortuary, wodi ya wazazi na tutafanya ukarabati mwingine halafu tutawawekea vifaa. Vilevile eneo hili la pili tutaliangalia kwa sababu lengo letu kubwa ni wananchi wa Tunduru waweze kupata huduma nzuri ya afya kwa sababu tunafahamu Wilaya ya Tunduru kwa jiografia yake, changamoto ya afya ni kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mpakate kwamba ahadi na maombi yake tulipokuwa katika mkutano, tumeyatekeleza na tunaendelea kuyafanyia kazi kwa kadri iwezekanavyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved