Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ahmed Juma Ngwali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ziwani
Primary Question
MHE. AHMED JUMA NGWALI aliuliza:- Tanzania ilibadilisha Sera yake ya Kibalozi ili kuendana na mazingira ya sasa ya kiuchumi duniani kwa maana ya kujiwekeza katika Diplomasia ya Uchumi (Economic Diplomacy). (a) Je, ni lini Tanzania ilibadili Sera yake ya Mambo ya Nje ya awali na kujielekeza katika Sera ya Diplomasia ya Uchumi? (b) Je, mwenendo ukoje kati ya sera hii na ile iliyokuwepo awali? (c) Je, ni vigezo au vipimo gani vinavyotumika kupima Balozi zetu katika utekelezaji wa sera hii ya Diplomasia ya Uchumi.
Supplementary Question 1
MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa sababu tumetoka katika siasa ya uchumi na tumeingia katika sera mpya ya demokrasia ya uchumi, naomba niuize kwamba Serikali imejipanga vipi katika kuandaa wataalam katika kuhakikisha hiyo dhana halisi ya kufikia hiyo demokrasia ya uchumi inafikiwa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, nauliza kutokana na hali mbaya za Balozi zetu ambazo kila mmoja anaelewa nadhani kwamba Balozi zetu hazipo katika hali nzuri, Serikali imejipanga vipi kupeleka bajeti na kuhakikisha kwamba bajeti hiyo inatosha kwa ajili kuhudumia Balozi ili waweze hasa hiyo mikakati kwa ajili ya kutekeleza hiyo diplomasia ya uchumi? Ahsante.
Name
Dr. Susan Alphonce Kolimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza kuhusu Wizara imejipangaje katika kuandaa wataalam ambao wataweza kutekeleza diplomasia ya uchumi; kama tulivyokuwa tumeeleza katika hotuba yetu ya bajeti, katika mpango wetu wa bajeti, katika kila Kitengo cha Wizara tumeweka sehemu ambayo inaangalia mafunzo ya watumishi wetu na katika kila kitengo inaangalia kwamba ina idadi ya watumishi wangapi na wangapi watatakiwa kwenda kwenye training na training hizo zinaendelea.
Mheshimiwa Spika, mafunzo haya yanafanywa nje na ndani ya nchi. Kuna semina mbalimbali, wanahusishwa katika ushiriki wa Mikutano yetu ya Kimataifa, lakini vilevile wanapelekwa katika training ni za muda mrefu na zile za muda mfupi.
Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema katika utekelezaji wa diplomasia ya kiuchumi, haihusishi tu Wizara ya Mambo ya Nje, hili ni suala mtambuka, linagusa Wizara nyingine za kisekta na hata tunapojadili miradi ambayo imetafutwa kwa fursa kwa kupitia Wizara yetu, tunahusisha pia Wizara za kisekta na katika Wizara za kisekta tunatumia pia wataalam katika Wizara husika pamoja na Wizara yetu. Kwa hiyo, tumejipanga vizuri kama Serikali.
Mheshimiwa Spika, katika suala la pili ambalo linahusu mkakati wa kusimamia na kuhakikisha kwamba bajeti iliyopangwa inakwenda; sisi kama Wizara tunajua kwamba tunawajibika, tunajua kuna watu ambao wanafanya kazi kwa ajili ya Serikali hii na kazi yetu kubwa kama Wizara ni kuhakikisha kwamba bajeti ambayo tumeiomba na imepitishwa katika Bunge hili inakwenda kwa wakati na tutakuwa tunaendelea kufuatilia.
Mheshimiwa Spika, pia katika siku zijazo tutaendelea pia kuliomba Bunge hili kuhakikisha kwamba wanapitisha bajeti ambayo tunaiomba ili kuhakikisha kwamba tunatekeleza hii diplomasia ya uchumi kwa ukamilifu zaidi.
Name
Ally Abdulla Ally Saleh
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Malindi
Primary Question
MHE. AHMED JUMA NGWALI aliuliza:- Tanzania ilibadilisha Sera yake ya Kibalozi ili kuendana na mazingira ya sasa ya kiuchumi duniani kwa maana ya kujiwekeza katika Diplomasia ya Uchumi (Economic Diplomacy). (a) Je, ni lini Tanzania ilibadili Sera yake ya Mambo ya Nje ya awali na kujielekeza katika Sera ya Diplomasia ya Uchumi? (b) Je, mwenendo ukoje kati ya sera hii na ile iliyokuwepo awali? (c) Je, ni vigezo au vipimo gani vinavyotumika kupima Balozi zetu katika utekelezaji wa sera hii ya Diplomasia ya Uchumi.
Supplementary Question 2
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, je, anaweza kutueleza hapa kwamba kuna chuo chochote kile ambacho kinaendesha kozi ya ubobezi ya diplomasia ya kiuchumi hivi sasa? Kama hakipo, je, Serikali ipo tayari kutumia nafasi yake kushawishi specifically kuendesha kozi hizo bobezi katika kiwango cha Masters na Ph.D ili tupate hao watalaam wanaotakiwa? (Makofi)
Name
Dr. Susan Alphonce Kolimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Spika, vyuo vya ubobezi wa diplomasia viko vingi, lakini kama nilivyosema kwenye majibu ambayo niliongezea katika maswali ambayo ameuliza Mheshimiwa Ngwali, nimesema kwamba katika bajeti ya Wizara, katika vitengo vyetu tumepanga bajeti ya kuhakikisha kwamba hao watumishi wanapata mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu na mafunzo haya wanayapata kutoka kwenye Chuo cha Diplomasia, vilevile wanapata nje ya nchi ambako kuna mafunzo ambayo ni ya ubobezi pia.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Ally Saleh kwamba jambo hili Wizara inalitambua.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved