Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
George Malima Lubeleje
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Serikali ilikuwa na mpango wa kuanzisha Kata mpya ya Mkanana ambayo ina vijiji vya Mkanana na Chibwegele na vipo mlimani ambapo hakuna huduma yoyote kama vile barabara ambayo ni mbaya sana na hupitika kwa shida wakati wote. Je, mpango huo wa kuanzisha Kata mpya umefikia wapi? Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba kuanzishwa kwa kata hiyo kutawezesha kuwasogezea karibu huduma mbalimbali wananchi wa kata hiyo kuliko ilivyo sasa ambapo Makao Makuu yapo Kijiji cha Chitemo, umbali wa kilometa 45?
Supplementary Question 1
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Kwanza utaratibu wote umeshafuatwa, vijijji vimekaa, Kamati ya Maendeleo ya Kata imekaa, Full Council imekaa na mpaka kwenye Kamati ya Ushauri ya Mkoa na ni ombi la muda mrefu sana. Wananchi wa Mkanana wanapata shida, kwanza hakuna mawasiliano ya barabara kabisa na ninakuomba tukimaliza Bunge tuende kule upite ile njia uone kama inapitika.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, kwa kuwa kwenye swali langu limetaja kuna umbali kutoka Mkanana, Chibwegele mpaka Chitemo ni kilometa 45 ndipo wananchi wanafuata usafiri. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, utakuwa tayari kukubali ombi langu tufuatane na wewe sasa baada ya Bunge hili, ukawaone watu wa Mkanana, Chibwegele, wanavyopata shida?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwanza nikiri nipokee kama taratibu zote mpaka katika ngazi ya mkoa zimekamilika tutafanya ufuatiliaji kuangalia utaratibu umefanyika lini. Kama sio yale maombi ya zamani ambayo mwanzo yalikuwa hayakukizi vigezo, kama haya mapya, ofisi yangu nadhani inafanya uchambuzi wa maeneo mbalimbali katika maeneo haya mapya.
Mheshimiwa Spika, lakini katika jambo lingine la pili, Mheshimiwa mbunge ameomba ikiwezekana twende pamoja, naomba nikueleze wazi na mimi niko pamoja kwa sababu, najua Mheshimiwa Mzee Lubeleje watu, wanahistoria hawafahamu kwamba Mpwapwa yote ilikuwa Jimbo moja wakati huo, baadaye ikagawanyika na Jimbo lingine la Kongwa. Kwa hiyo, alifanya juhudi hizi miaka mingi sana katika michakato mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niwahakikishie Wana-Mpwapwa, Wana-Kongwa na sehemu uliyosema, tutafika pale tutabaini miongoni mwa mambo hayo, lakini hasahasa tatizo la barabara katika Wilaya ya Kongwa na Wilaya ya Mpwapwa, nini tufanye kwa pamoja kuwasaidia wananchi hawa ambao kwa kiwango kikubwa wameisaidia sana Serikali hii katika mambo mbalimbali.
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Serikali ilikuwa na mpango wa kuanzisha Kata mpya ya Mkanana ambayo ina vijiji vya Mkanana na Chibwegele na vipo mlimani ambapo hakuna huduma yoyote kama vile barabara ambayo ni mbaya sana na hupitika kwa shida wakati wote. Je, mpango huo wa kuanzisha Kata mpya umefikia wapi? Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba kuanzishwa kwa kata hiyo kutawezesha kuwasogezea karibu huduma mbalimbali wananchi wa kata hiyo kuliko ilivyo sasa ambapo Makao Makuu yapo Kijiji cha Chitemo, umbali wa kilometa 45?
Supplementary Question 2
MHE. ALPHAXARD K. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri alishuhudia mgawanyo wa majimbo mawili ya Bunda na Mwibara kutokutana ndani ya Halmashauri moja. Na kwa kuwa, Mheshimiwa Waziri wa wakati huo, Mheshimiwa Simbachawene alikuja kushuhudia na kuamua kwamba, wabadilishe mipaka Jimbo la Bunda lirudi Bunda Mjini wawe Halmashauri moja na Mwibara ibaki yenyewe iwe halmashauri wakatuahidi watatoa Government Notice muda si mrefu na ilikuwa mwezi wa saba. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, hiyo GN imefikia hatua gani, Wana-Mwibara wanataka kusikia?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni kweli analozungumza Mheshimiwa Mbunge hapa hazushi na bahati nzuri mimi nimepata fursa ya kutembelea majimbo haya yote matatu, Jimbo la Mwibara, Jimbo la Bunda Vijijini, hali kadhalika Jimbo la Bunda Mjini. Mgawanyiko wake kwa kweli, ulikuwa una changamoto kubwa sana na bahati nzuri harakati hizi zimeshaanza.
Naomba nichukue ombi lako hili Mheshimiwa Kangi, twende tukalifanyie kazi kwa undani kujua kwamba, hili jambo limefikia wapi na hasa taratibu zilizofuatwa pale, baadaye tutaweza kutoa maamuzi sahihi, lakini sitaki kutoa commitment ya moja kwa moja hapa, tunalifahamu hili jambo tutaenda kulifanyia kazi kwa maslahi mapana ya hizi halmashauri zetu ambazo ziko kule.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved