Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Allan Joseph Kiula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanasababisha vifo vingi, hasa kwa Watanzania wanaoishi vijijini ambako madaktari bingwa na huduma za vipimo vya maabara havipatikani:- • Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha programu maalum ya kupeleka Madaktari Bingwa na maabara zinazotembea vijijini? • Je, Serikali ina mpango wa kutoa ruzuku ya tiba kwa Watanzania wasio na uwezo wanaougua magonjwa yasiyoambukizwa?

Supplementary Question 1

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Waziri, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa sababu kampeni ilizinduliwa tangu mwaka 2016 mpaka leo ni mikoa mitano tu na maeneo mengi yaliyofikiwa yana hospitali kubwa kama Muhimbili, KCMC, sasa ni lini kampeni hiyo itafika katika Mkoa kama wa Singida, Wilaya ya Mkalama na mikoa mingine maeneo ya vijijini kwa sababu vifo vinaendelea kutokea kwa kasi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali itawathibitishia vipi Watanzania, wakiwemo wananchi wa Mkalama, kwamba Serikali inagharamia matibabu kufuatia jibu la Waziri, kwa sababu mimi ni mhanga, mwananchi…
Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itawathibitishia wananchi kugharamia matibabu ya kansa? Mkalama kuna mwananchi amepoteza maisha kwa kukosa dawa.

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, ni kwamba tumetengeneza ratiba. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge avute subira, muda utakapofika kwa Mkoa wa Singida nimwombe atoe ushirikiano ili zoezi hili liwe la mafanikio.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili ambalo lilikuwa linauliza Serikali imejipangaje kuhusiana na masuala ya upatikanaji wa dawa; napenda kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali katika mwaka huu wa fedha imeongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni 260.
Mheshimiwa Spika, napenda kumhakikishia, hadi hivi sasa, hali ya upatikanaji wa dawa za kansa ni zaidi ya asilimia 80 na vilevile, hospitali kama ya Ocean Road imefungua dirisha la dawa ambapo dawa nyingine ambazo hazipatikani pale zinapatikana kwa gharama nafuu kuliko katika maduka mengine ya dawa.

Name

Rhoda Edward Kunchela

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanasababisha vifo vingi, hasa kwa Watanzania wanaoishi vijijini ambako madaktari bingwa na huduma za vipimo vya maabara havipatikani:- • Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha programu maalum ya kupeleka Madaktari Bingwa na maabara zinazotembea vijijini? • Je, Serikali ina mpango wa kutoa ruzuku ya tiba kwa Watanzania wasio na uwezo wanaougua magonjwa yasiyoambukizwa?

Supplementary Question 2

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tatizo la Iramba Mashariki linafanana kabisa na matatizo ambayo yako katika Mkoa wa Katavi. Uhaba wa Madaktari Bingwa katika Mkoa wa Katavi umekuwa ni changamoto kubwa sana, kwa mfano katika Kata za Mishamo, Chamalendi, Kakese pamoja na Mwamkulu, ni maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za Madaktari na wanapopewa rufaa kwenda katika Mikoa ya Mbeya pamoja na Dar es Salaam inawagharimu gharama kubwa za kuishi pamoja na za madawa. Sasa nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wanaharakisha tunapata Madaktari Bingwa katika Mkoa wa Katavi?

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, nakiri kwamba tumekuwa na changamoto kidogo katika upatikanaji wa Madaktari Bingwa, lakini hivi karibuni tumepata kibali cha kuajiri wataalam wapya wa afya na Mkoa wa Katavi ni mmoja k atika mikoa ambayo imepata Madaktari hao.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, katika kipindi cha mpito, tumeongeza udahili katika fani za Madaktari Bingwa, lakini vilevile tumekuwa tunaendesha mobile clinics kwa ajili ya kuwapeleka wale wataalam wachache katika mikoa iliyo pembezoni kwa ajili ya kupata huduma hizo.