Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Maryam Salum Msabaha
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Majengo ya Kituo Afya cha Kambi ya Jeshi Migombani Unguja ni chakavu na pia ni siku nyingi sana. Je, ni lini Serikali itajenga kituo hicho ili kiwe cha kisasa na kiendane na wakati?
Supplementary Question 1
MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Naibu Spika, asante kwa kuwa haya maswali tumekuwa mara kwa mara tunauliza na hakuna utekelezaji. Je, naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri nusu mwaka wa fedha unakwishwa. Ni majengo mangapi yamekarabatiwa kwa upande wa Zanzibar na ni vituo vingapi vya kambi vya Kambi za Jeshi kwa upande wa Zanzibar vimekarabatiwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuwa hivi vituo vya afya tunavyoviulizia ambavyo vipo kwenye makambi ya Jeshi havihudumii tu majeshi na familia zao, zinahudumia pia na jamii zilizowazunguka na hasa hichi kituo nilichokiulizia kiko sehemu ambapo ajali zinatokea mara kwa mara.
Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha vituo vyote vya majeshi vinapata dawa kwa wakati muafaka na sitahiki zinazofaa kwa wakati muafaka? Ahsante.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI (K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nilivyojibu katika majibu ya msingi kwamba kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 Serikali imeazimia kuvifanyia ukarabati vituo vyote ikiwemo vya Zanzibar na kikiwemo hiki cha kwenye Brigedi ya Nyuki, Migombani. Kwa hiyo, mwaka wa fedha 2018/2019 bado haujaisha kadri ambavyo fedha kama ambavyo nimesema zitapatikana basi vituo hivi pamoja na hiki cha Migombani vitafanyiwa ukarabati. Sambamba na kuvipatia huduma nyingine muhimu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa kwa hatua za awali.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ikumbukwe kwamba vituo hivi kwa kawaida vinatumika kwa ajili ya kutoa huduma za awali kabla ya kuweza kuwapeleka wagonjwa wenye matibabu makubwa katika Hospitali za Kikanda kwa upande wa Zanzibar ikiwemo Hospitali ya Jeshi ya Bububu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved