Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJENZA aliuliza:- Kuna mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya TANAPA na Wananchi wa Kata za Ilungu, Igoma, Uleuje na wananchi walikuwa tayari kuachia ardhi yao ili upanuzi wa Hifadhi ya TANAPA lakini Serikali imeshindwa kuwalipa wananchi hao fidia:- (a) Je, ni lini Serikali itafanya tathmini mpya ya fidia kwa wananchi wa Ilungu, Igoma na Uleuje? (b) Kama Serikali imeshindwa kulipa fidia; je, ni lini itarudisha eneo hilo kwa wananchi wa Kata hizo?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJENZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, napenda vile vile kushukuru majibu ya Serikali na pia nipende kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya mkoa na TANAPA vile vile kwa kushiriki katika ujenzi wa kituo cha afya pale Ilungu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kwa vile hii fidia ni ya muda mrefu 1965; je, Serikali inathibitisha kuwa hii fidia itakayolipwa mwaka huu itazingatia thamani na sheria zilizopo sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa vile Mji wa Mdogo wa Igoma unakua kwa haraka sana na pale kuna eneo la hifadhi ambalo limezungukwa na mji; je, Serikali itakuwa tayari kuliachia lile ili liweze kutumiwa na shule pamoja na huduma zingine za kijamii? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijajibu hilo swali, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya katika kufuatilia fidia hii ya wananchi wake na amefuatilia kwa muda mrefu na taarifa ziko nyingi sana na wananchi wajue kwamba Mheshimiwa Mbunge anafanya kazi nzuri sana hongera sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu fidia, kama nilivyosema kwenye swali la msingi tunafanya tathimini upya mwezi Februari mwaka huu. Kwa hiyo, baada ya tathimini hiyo ni wazi kabisa kwamba tutabaini kwamba mahitaji au fidia inayotakiwa italingana na hali halisi ya leo na si ya mwaka 1965. Kwa hiyo wananchi watapata nafasi nzuri kabisa ya kupata fidia inayostahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maombi yanayohusu hapa kujenga makao makuu kutokana na ongezeko la watu. Naomba nitoe maelezo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza maeneo mengi yameleta maombi ya namna hiyo yanayofanana, lakini hili ombi ambalo amelileta Mheshimiwa Mbunge nimhakikishie tu nitachukua jukumu la kwenda kwanza kukutana na wananchi wenyewe ili niangalie hilo eneo kama kweli linafaa kutolewa kwa ajili ya huduma za jamii. Hata hivyo, mkazo zaidi utaendelea kusisitizwa kwamba hifadhi ni muhimu kuliko vitu vingine vyote.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved