Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE: RASHID A. SHANGAZI aliuliza:- Tanzania imeridhia na kuingia mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo diplomasia na mahusiano. Je, ni nchi ngapi na zipi ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea moja kwa moja kwa utaratibu wa visa on entry wakati wa kuingia ukiondoa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki?
Supplementary Question 1
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante, majibu ya Wizara yanaonekana ni mepesi sana kwa sababu nchi nyingi anazozitaja ni nchi za kiafrika na lengo mahususi ya hili swali tulikuwa tunataka tujue nchi zote ulimwenguni lakini natambua kwamba nchi zilizopo chini ya Umoja wa…
Nchi zilizopo chini ya Umoja wa Madola (Commonwealth) tuna utaratibu huu wa visa on entry or visa on arrival. Je, kwa nini wananchi wa India wanapokuja Tanzania wanakuja kwa visa on arrival, lakini sisi tunapokwenda nchi kama India lazima uombe visa hasa ikichukuliwa kwamba Watanzania wengi wanakwenda India kwa ajili ya kupata huduma za matibabu?
Swali la pili, zipo nchi za Afrika Magharibi ambazo wanaingia kwa visa ya referred visa ikiwemo Cote d’voire, Senegal na Mali. Je, kwa nini sasa isiwe ni wakati muafaka wa kuiunganisha Nigeria katika nchi hizi kwasababu inaonekana kwamba mara nyingi wanapoingia huku kwetu wanahatarisha usalama wa nchi?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nchi za Jumuiya ya Madola zina utaratibu wa wananchi wake kutembeleana bila visa. Lakini kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba ushirikiano na matengamano hayo ikiwemo la Jumuiya ya Madola, utaratibu wake unaweza kubadilika kulingana na mahusiano pamoja na hali za kiusalama. Kwa hiyo, sio jambo la kushangaza kuona India na Nigeria juu ya kwamba zote mbili ni wanachama wa Jumuiya ya Madola lakini utaratibu wa visa on arrival ukawa hautumiki.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved