Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI (K.n.y MHE. ESTHER L. MIDIMU) aliuliza:- Barabara za Vijiji katika Wilaya ya Maswa ni mbovu kiasi kwamba sehemu nyingi za maeneo ya vijijini hayapitiki. Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha za kutosha za Mfuko wa Barabara ili barabara hizo zifanyiwe matengenezo?

Supplementary Question 1

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa, pesa hizi za Mfuko wa Barabara zinapelekwa kidogo kidogo, kwa mwezi au baada ya miezi kadhaa. Je, Serikali haioni kuna sababu sasa ya kupeleka fedha hizi kwa mkupuo ili Halmashauri iweze kupangilia vizuri ujenzi na ukarabati wa barabara zake kwa umakini zaidi kuliko hivi sasa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo ni zuri lakini kama mnavyofahamu tunakwenda kwa utaratibu wa cash budget, kadri tunavyopata, tunavyokusanya pesa hizi za barabara ndiyo tunazipeleka hivyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba aondoe hofu Serikali itajitahidi kwa kadri iwezekaavyo na kwa sababu tumejielekeza vizuri katika makusanyo ya mapato, nina imani katika Jimbo lake na najua kwamba katika Mji wake wa Mwasa ana ahadi ya ile barabara ya Mheshimiwa Rais ya kilometa tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka huu barabara hiyo tumeiingiza katika mpango wa bajeti barabara ile ya one point something billion itaingia pale. Kwa hiyo, naomba niwahakikishie kwamba tutajitahidi kukusanya fedha na kuhakikisha kwamba commitment zote za Serikali tulizoziweka ziweze kutekelezeka katika Majimbo.