Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
George Malima Lubeleje
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y. MHE. HASNA S. K. MWILIMA) aliuliza:- Kituo cha Afya cha Nguruka kinahudumia Wakazi wa Kata Nne za Tarafa ya Nguruka pamoja na wananchi wa Usinge katika Wilaya ya Kaliua. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho kwa kuongeza miundombinu na kumalizia ukarabati wa jengo la Mama na Mtoto ambalo limeachwa bila kukarabatiwa kwa muda mrefu?
Supplementary Question 1
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Swali hili linafanana kabisa na vituo vya afya vya Mima na Mbori ambavyo havijakamilika sasa ni zaidi ya miaka 10 lakini naishukuru Serikali kwamba mmetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha vituo hivyo. Sasa Mheshimiwa Waziri utakuwa tayari kutembelea kuona ujenzi wa kituo cha afya - Mima na kituo cha afya cha Mbori?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa kuna mpango wa kujenga kituo cha afya Chunyu na eneo la Chunyu lina idadi ya watu wengi, je, mpango huu umefikia wapi? Ahsante.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje, greda la zamani makali ya yale yale kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, niko tayari kutembelea kituo cha afya Mima na Mbori, tumekubaliana na Mheshimiwa Mbunge licha ya vituo hivi vya afya, tutakwenda kutembelea na miundombinu ya barabara katika Jimbo lake ambalo kwa kweli lina mtandao mkubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, katika kituo cha afya hicho ambacho ameuliza kwamba mpango ukoje, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tukishafika site sasa japo tutatembelea vituo hivi vya afya viwili, lakini ni vema tutembelee na kituo cha afya hiki kipya ambacho kiko katika mpango wa ujenzi halafu pale tutajadiliana kwa pamoja nini tufanye ili wananchi wa kituo hiki kiweze kujengwa na wananchi wa eneo lile waweze kupata huduma.
Name
Magdalena Hamis Sakaya
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Kaliua
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y. MHE. HASNA S. K. MWILIMA) aliuliza:- Kituo cha Afya cha Nguruka kinahudumia Wakazi wa Kata Nne za Tarafa ya Nguruka pamoja na wananchi wa Usinge katika Wilaya ya Kaliua. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho kwa kuongeza miundombinu na kumalizia ukarabati wa jengo la Mama na Mtoto ambalo limeachwa bila kukarabatiwa kwa muda mrefu?
Supplementary Question 2
MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri swali moja dogo la nyongeza. Kwa kuwa, wananchi wa Kata ya Usinge Wilaya ya Kaliua wanakwenda Nguruka kwa sababu Kata ya Usinge ambayo ni kubwa sana ina wananchi wengi na ni center ya biashara haina kituo cha afya, ina Zahanati moja ndogo kiasi ambapo inasababisha watu waende kule Nguruka ambapo ni mbali sana karibu kilometa 40 kwenda pale Nguruka. Je, Serikali ina mpango gani sasa kuhakikisha ule mpango wake wa kujenga kituo cha afya Kata ya Usinge unaanza haraka ili kupunguza msongamano wa wananchi wanaokwenda kuhudumiwa katika Kata ya Nguruka? Ahsante.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Kata ya Usinge ina changamoto kubwa na ukiangalia population pale ni kubwa sana, wakati ukitoka Kigoma pale ukipita unaona kweli kuna haja. Naomba niseme kwamba Serikali tumelichukua hili, tutahakikisha tunafanya kila liwezekanalo eneo lile kujenga kituo cha afya ili wananchi waweze kupata huduma.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y. MHE. HASNA S. K. MWILIMA) aliuliza:- Kituo cha Afya cha Nguruka kinahudumia Wakazi wa Kata Nne za Tarafa ya Nguruka pamoja na wananchi wa Usinge katika Wilaya ya Kaliua. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho kwa kuongeza miundombinu na kumalizia ukarabati wa jengo la Mama na Mtoto ambalo limeachwa bila kukarabatiwa kwa muda mrefu?
Supplementary Question 3
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kuna mpango wa kujenga vituo vya afya 100 ambao tumeusikia kwa muda mrefu sana na mojawapo ni kituo cha kwangu cha Mgeta. Sasa ningependa kujua ni kigugumizi gani kipo mpaka sasa vituo vile havijaanza kujengwa wakati hela imetoka muda mrefu?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna mpango wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya na miongozi mwa vituo hivyo ni Kituo cha Afya cha Mgeta. Naomba niwaambie kwamba mchakato sasa uko katika suala zima la evaluation, tulikuwa katika tendering process kwa sababu tuna vituo vingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika kipindi hiki cha mwezi wa Julai wataona ujenzi unaendelea katika maeneo mbalimbali ya vituo vile 100; then tutakuwa na program nyingine ya ujenzi wa vituo vipatavyo 42. Kwa hiyo, kuanzia mwezi wa Julai wananchi wa Mgeta watarajie kwamba, ujenzi katika eneo lao utaanza mara moja.
Name
Mwanne Ismail Mchemba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y. MHE. HASNA S. K. MWILIMA) aliuliza:- Kituo cha Afya cha Nguruka kinahudumia Wakazi wa Kata Nne za Tarafa ya Nguruka pamoja na wananchi wa Usinge katika Wilaya ya Kaliua. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi kituo hicho kwa kuongeza miundombinu na kumalizia ukarabati wa jengo la Mama na Mtoto ambalo limeachwa bila kukarabatiwa kwa muda mrefu?
Supplementary Question 4
MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa kituo cha afya cha Manonga kimekamilika na kwa kuwa mpaka sasa vifaa havijapelekwa. Je, ni lini sasa Mheshimiwa Waziri watapeleka vifaa hivyo kwa ajili ya wodi ya upasuaji?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kituo cha afya cha Manonga kimekamilika na nakumbuka vituo vile vilikuwa ni miongozi mwa vituo ambavyo tumetengeneza kwa African Developmnet Bank na vituo vile tulitengeneza pale Bukene katika Mkoa wake, hali kadhalika hapa Itogo, lakini bahati mbaya Manonga vifaa vilikuwa havijafika, hata kwa ndugu yangu Mheshimiwa Cecil Mwambe pale kulikuwa na kazi tumefanya katika kituo cha Chiwale, vinafanana katika kesi kama hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Manonga kulikuwa na kesi maalum kwamba vifaa havikufika na kwa sababu jambo lile lilikuwa na bajeti yake maalum, naomba niseme kwamba tunalichukua na tutalifanyia kazi kwa haraka sana kwa sababu bajeti yake ilikuwepo ili vifaa vile viweze kufika, wananchi wa Manonga waweze kupata huduma kama ilivyokusudiwa katika mradi ule.