Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwantakaje Haji Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Bububu
Primary Question
MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itawapatia gari lingine Kituo cha Polisi Magharibi ‘A’ ili kupunguza matumizi ya magari binafsi kwa Jeshi la Polisi? (b) Je, Serikali imejipanga vipi kupunguza uhalifu unaojitokeza mara kwa mara?
Supplementary Question 1
MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa fungu la mafuta katika magari hayo linakuwa ni kidogo, je, ni lini Serikali itaongeza mafuta hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili katika Mkoa wangu wa Magharibi ‘A’ mafuta wanapokea kwa siku lita saba au hawapokei kabisa, je, ni lini Serikali itawaongeza mafuta hayo? Ahsante (Makofi)
Name
Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Magharibi
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia kwa ukaribu sana mazingira ya kazi ya askari wetu na kwa kweli watu wa Bububu hawakukosea na mimi mwenyewe nilishafika Bububu nikaona hali ya uhitaji wa usalama unavyohitajika.
Mheshimiwa Spika, niseme tu katika muhula kwanza, katika mwaka wa fedha uliopita nusu mwaka ya kwanza ukilinganisha na nusu mwaka ya pili utaona kwamba bajeti ya mafuta iliongezeka. Katika bajeti tuliyoipitisha fedha ambazo tulitenga kwa ajili ya mafuta ziliongezeka. Nashukuru wenzetu wa Wizara ya Fedha wamekuwa wakizitoa fedha hizo ambazo zinaenda kwa ajili ya mafuta ili kuweze kuwezesha vijana wetu waweze kufanya doria kikamilifu. Kwa hiyo jambo hilo litafanyiwa kazi tunavyomaliza bajeti ili waweze kupata fedha hizo waweze kufanya doria kikamilifu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved