Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Wilaya ya Itilima na Busega ni Wilaya mpya na hazina Hospitali za Wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya kwenye Wilaya hizo?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza kabisa, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri yaliyojitosheleza. Pia naishukuru Serikali yangu kwa kutenga hizo shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya za Itilima na Busega. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niulize swali la nyongeza; kwa kuwa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu jengo la OPD lipo tayari na maelezo ya mkandarasi ambaye ni TBA amesema jengo hilo litakabidhiwa tarehe 28 Mei, 2018 kwa Katibu Tawala wa Mkoa. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuweza kutujengea wodi ya wazazi, watoto, wanawake na wanaume ili hospitali hiyo ianze kazi haraka? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Hospitali Teule ya Mkoa haina kabisa gari la kubebea wagonjwa kupeleka Hospitali ya Rufaa Bugando, gari lililopo wanatumia hardtop almaarufu chai maharage; je, ni lini Serikali itatuletea gari la kubebea wagonjwa kupeleka katika Hospitali ya Rufaa. (Makofi)
Name
Dr. Faustine Engelbert Ndugulile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigamboni
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya Wizara ya Afya ambayo tumeipitisha hivi karibuni, Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikao ya Katavi, Njombe, Simiyu, Songwe na Mara. Kwa hiyo, Hospitali ya Simiyu ni sehemu ya hospitali ambazo zitaendelezwa kujengwa katika mwaka huu wa fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba ya hilo, Serikali imeagiza ambulances na zitakapofika Mkoa wa Simiyu utakuwa ni mmoja ya mkoa ambao tutaufikiria kupata ambulance. (Makofi)
Name
Mary Pius Chatanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Wilaya ya Itilima na Busega ni Wilaya mpya na hazina Hospitali za Wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya kwenye Wilaya hizo?
Supplementary Question 2
MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Korogwe hususan Korogwe Mjini tuna Hospitali ya Magunga, lakini tuna kata mbili ambazo zipo mbali nje ya mji kabisa, Kata ya Kwamsisi na Kata ya Mgombezi ambazo zina vijiji kama sita sita. Je, Serikali itakuwa tayari kutusaidia kupata fedha kwa ajili ya kuwajengea vituo vya afya? (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo imeelekezwa kwenye Ilani ya CCM kwamba Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kwamba tunajenga vituo vya afya kila kata, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni suala tu la bajeti na safari ni hatua. Yeye mwenyewe ni shuhuda jinsi ambavyo tumeanza ujenzi wa vituo vya afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaamini kabisa wakati mwingine hatua nyingine itafika mahali ambapo hizo kata ambazo zipo mbali zitafikiwa kwa sababu ndiyo azma ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Wilaya ya Itilima na Busega ni Wilaya mpya na hazina Hospitali za Wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya kwenye Wilaya hizo?
Supplementary Question 3
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Sera ya Afya inazungumzia zahanati kwa kila kijiji, vituo vya afya kwa kila kata na hospitali za wilaya katika wilaya, jambo ambalo sera hii haijakamilika hasa katika Mkoa wetu wa Rukwa ambao hauna Hospitali ya Wilaya hata moja, ni lini sera hii itakamilika kikamilifu hasa katika Mkoa wetu wa Rukwa?
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimetoka kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mary Chatanda na Mheshimiwa Khenani ni shuhuda kwamba miongoni mwa Wilaya 67 ambazo zinaenda kujengewa Hospitali za Wilaya, ni pamoja na Wilaya ya Kalambo, Sumbawanga Vijijini pamoja na Wilaya ya Nkasi. Sasa siyo rahisi kusema lini exactly kwa sababu na ujenzi nao ni process, lakini na yeye mwenyewe ni shuhuda jinsi ambavyo Serikali imeazimia na inatekeleza.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved