Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Serikali imeanzisha Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kwa lengo la kutatua matatizo ya walimu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuimarisha Tume hiyo ili ifanye kazi kikamilifu kama ilivyokusudiwa?
Supplementary Question 1
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuimarisha Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC), kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili walimu na matatizo mengi.
Swali la kwanza, ni kwamba, je, Serikali iko tayari kuwatuma wataalam kwa mfano Kenya kwenda kujifunza jinsi ambavyo wenzetu wameweza kuimarisha chombo kama hiki cha TSC ili kifanikishe katika utoaji wa huduma kwa walimu kwa kuwa nao Kenya walikuja kujifunza kutoka kwetu, wao wakaenda wakaimarisha wakafanikisha?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali iko tayari baada ya kuwatuma wataalam Kenya kujifunza jinsi ambavyo wamefanikisha wenzetu, kurudi huku na wahakikishe kwamba, wanachukua hatua za kuimarisha, ili kifanikishe katika kutoa huduma kwa walimu?
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nieleze kidogo kuhusu Mheshimiwa Mama Margaret Sitta. Mheshimiwa Sitta ni hazina kubwa ya kumbukumbu na uzoefu katika sekta ya elimu nchini kama Mwalimu, Afisa Elimu, Kiongozi wa Chama cha Walimu, Waziri na Mbunge. Kwa hiyo, kwa kweli, amekuwa msaada mkubwa sana kwetu Serikali katika kutoa mawazo ya kuiboresha zaidi sekta ya elimu na sisi tutaendelea kufaidika nayo.
Mheshimiwa Spika, sasa naomba nijibu maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo, kwa pamoja:-
Mheshimiwa Spika, kwamba ushauri wake wa kwenda kujifunza katika nchi ya Kenya tumeupokea na tutaufanyia kazi. Mapendekezo na ushauri wake katika suala la pili nao tunaupokea na tutaufanyia kazi, ili kuboresha zaidi Tume ya Utumishi wa Walimu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved