Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Alfredina Apolinary Kahigi
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALFREDINA A. KAHIGI aliuliza:- Madarasa na Ofisi za Walimu katika shule mbalimbali katika Mkoa wa Kagera ni mabovu. Je, Serikali inawasaidiaje wanafunzi wa Kagera kupata mahali pazuri pa kusomea kadhalika na walimu wao wapate ofisi nzuri ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa?
Supplementary Question 1
MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, ni lini Serikali itawajengea nyumba walimu wale ambao hawana nyumba kabisa katika shule zao? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa mambo mazuri yanaigwa, je, Wakuu wa Mikoa hawaoni kama ni vizuri kumuiga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Makonda nao waweze kutafuta wafadhili wa kuweza kuwajengea walimu nyumba za kuishi na ofisi? Ahsante. (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la upungufu wa nyumba za walimu, naomba nimsihi Mheshimiwa Mbunge kwamba katika hizo pesa ambazo zimeletwa za EP4R ni wajibu wa halmashauri husika kuangalia kama hitaji kubwa ni nyumba za walimu, hakuna dhambi pesa hizo zikatumika pia katika kuhakikisha nyumba zinajengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, naamini ni wazo jema, naomba niwasihi Wakuu wa Mikoa mingine waige mfano mzuri kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge yeye mwenyewe ameliona na anapongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved