Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Raphael Masunga Chegeni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busega
Primary Question
MHE. DKT. RAPHAEL M.CHEGENI aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwepo na migogoro mingi kati ya Hifadhi za Taifa na wananchi ambao ni wakulima na wafugaji hali inayosababisha uvunjifu wa amani:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa tatizo hili linapata ufumbuzi endelevu hasa maeneo ya Lamadi, Makiloba, Kijereshi na Nyamikoma katika Wilaya ya Busega? (b) Baadhi ya wanyama kama tembo wamekuwa wakifanya uharibifu wa mali na mazao ya wananchi wanaoishi maeneo hayo. Je, Serikali inatoa tamko gani la kuzuia tatizo hilo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, katika majibu yake amekiri tatizo la tembo linazidi kuongezeka na wananchi wengi sana wanapata madhara makubwa na wanaathirika sana na tatizo hili. Wananchi wa vijiji husika wakiwemo vya Matongo, Mwauchumu, Longalombogo na maeneo mbalimbali hapa nchini wameathirika sana. Nataka tu kujua Serikali sasa inachukua hatua gani za kimkakati, tuache hizi hadithi za kwamba tutafanya, tuko mbioni, ni lini tatizo hizi sasa tutalipatia ufumbuzi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Kikosi dhidi ya Ujangili kimeshajenga kituo pale Lukungu na kituo hiki maana yake ni kusaidia kufukuza wanyama waharibifu wakiwemo viboko. Je, ni lini kituo hiki cha Lukungu kitaanza kufanya kazi? (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Chegeni. Kwanza kabla sijajibu, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia na hii ni mara ya tatu kuliuliza hili swali, hii inaonesha kwamba hili swali ni muhimu sana katika eneo la Jimbo lake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema kwenye jibu la msingi kwamba katika maeneo yote haya ambayo kuna matatizo sasa hivi tutachukua hatua za dhati kuanzia tarehe 1 Julai, 2018 wakati bajeti mpya itakapoanza kutekelezwa. Tumejipanga sawasawa kuhakikisha kwamba haya yote tutayatatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu hiki Kituo cha Kupambana na Ujangili (KDU) kwanza kama alivyosema mwenyewe tayari majengo yameshakamilika, tunachosubiri hivi sasa ni kuhakikisha kwamba rasilimali watu pamoja na vifaa vya kutendeakazi vinakamilika ili kusudi kile kituo kianze kufanya kazi katika mwaka wa fedha unaokuja.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved